Takriban maafisa 302 wa polisi wamefutwa kazi nchini Kenya kwa kukataa kukaguliwa tangu mpango huo wa kutaka kukabiliana na ufisadi kuanzishwa mwaka 2013,kulingana na tume inayotekeleza ukaguzi huo.

Hayo yalibainishwa na Jonhston Kavuludi ,anayeongoza tume hiyo ya huduma za maafisa wa polisi huku maafisa wa polisi wakijiandaa kuhojiwa na jopo katika mji wa magharibi wa Kisumu.
Ukaguzi huo ni mpango wa uma na hufanywa mbele ya kamera ambapo maafisa uhojiwa kuhusu mali na fedha wanazomiliki huku mgongano wowote wa maslahi ukichunguzwa.
Mwezi uliopita wakati jopo hilo lilipokuwa Mombasa ,afisa mmoja wa idara ya trafiki hakuweza kusema ni wapi alipata takriban dola 500,000 ambazo ziliwekwa katika mtandao wa simu unaotuma fedha ama kupokea na akaunti yake ya benki.
Wakenya katika mitandao ya kijamii walishangazwa na kuelezea vile wanavyolazimishwa kutoa hongo baada ya kukamatwa kwa makosa ya trafiki.