Makumi ya maelfu ya watu wanatarajiwa kumuaga aliyekuwa bondia shupavu Muhammad Ali nyumbani kwake katika mji wa Louisville huko Kentucky.
Bingwa huyo wa ndondi katika uzani mzito duniani na mwanaharakati alifariki siku ya Ijumaa akiwa na umri wa miaka 74.
Image copyrightGETTYImage captionMuhammad Ali
Umati mkubwa wa watu utachukua mwili wake na kuupitisha katika maeneo muhimu ya maisha yake kabla ya kuufanyia ibada.
Muingizaji Will Smith na aliyekuwa bondia Lenox Lewis watakuwa miongoni mwa wale watakaobeba jeneza lake ,huku aliyekuwa rais wa Marekani Bill Clinton akitarajiwa kutoa hotuba.
Image copyrightGETTYImage captionIbada ya mwili wa Muhammad Ali
Msafara wa jeneza lake utaanzia saa tatu saa za Marekani na kulipitisha jeneza hilo nyumbani kwake,katika kituo cha Ali,baadaye kupitishwa katika kituo cha makavazi ya watu weusi nchini Marekani na baadaye katika eneo la Muhammad Ali Boulevard.
Image captionMuhammad Ali
Miongoni mwa wale wanaotarajiwa kuhudhuria ibada ni rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan na mfamle Abdullah wa Jordan.
Rais Obama hatakuwepo,kwa kuwa anatarajiwa kuhudhuria sherehe ya kufuzu kwa mahafala ya mwanawe mkubwa Malia.Mshauri mkuu wa ikulu ya rais Valerie Jarret ambaye alimjua Ali atamwakilisha rais.
Image copyrightGETTYImage captionMuhammad Ali
Lennox Lewis aliyekuwa bondia wa uzani mkubwa dunia kabla ya kustaafu kwake amesema kuwa ni heshimu kubwa kwake kuorodheshwa miongoni mwa wale watakaobeba jeneza la marehemu huku akisema kuwa kumbukumbu za Ali hazitasaulika.
Image copyrightGETTY IMAGESImage captionNyumbani kwa Muhammad Ali
Ali alitaka ibada ya Janazah kuwa wakati wa mafunzo kulingana na Imam zaid Shakir alieongoza ibada hiyo.
Msomi wa Kiislamu Sherman Jackson alisema:Kufariki kwa Muhammad Ali kumetufanya tujisikie wapweke duniani.''Kitu kizima,kitu kikubwa na kinachovutia na kinachotoa uhakika wa maisha kimetuwacha''.
Image copyrightGETTY IMAGESImage captionLennox Lewis na Muhammad Ali
Baada ya kujiuzulu,uvumi ulianza kuhusu hali yake ya kiafya.Ugonjwa wa kutetetemeka mwili baadaye ulipatikana lakini Ali aliendelea kuwepo katika maeneo ya hadhara huku akipokewa vizuri kila anapoenda.
0 Comments