Na Mwandishi Wetu
MICHUANO ya Copa America inayoonekana moja kwa moja kupitia visimbuzi vya StarTimes Tanzania imefikia hatua ya robo fainali ambayo itaanza kutimua vumbi kesho Juni 16 mpaka 19.
Timu zilizotinga hatua hiyo ni Argentina, Chile, Mexico, Marekani, Venezuela, Peru, Colombia na Ecuador huku mashabiki wa soka wakishuhudia miamba ya soka ya timu za Brazil na Uruguay wenye nyota lukuki kama vile Luis Suarez, Edinson Cavani, Willian, Countinho na wengineo wakishindwa kuzisaidia timu zao.
Katika michuano hii ya kusisimua kikosi cha timu ya taifa cha Argentina kikiongozwa na mchezaji bora wa dunia mara tano, Lionel Messi, ambacho kinapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo kimeingia kwa kishindo hatua ya robo fainali baada kushinda michezo yote mitatu na kuongoza kundi D kwa alama tisa.
Kupitia chaneli za Sports Focus na World Football wateja na watanzania wanatazama michezo yote moja kwa moja huku wakiwa na nafasi ya kusinda zawadi mbalimbali kama vile vifurushi vya bure pamoja na pesa taslimu na safari kwenda Ujerumani kutazama mechi za Bundesliga za msimu ujao unaotarajiwa kuanza mwezi wa nane.
Akitoa ufafanuzi juu ya michuano hiyo Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amesema kuwa, “Mbali na kufurahia matangazo ya moja kwa moja ya mechi zinazochezwa nchini Marekani pia tuna kampeni inayoendelea ya ‘Tabiri na Ushinde’ inayoenedelea kupitia mitandao yetu ya facebook na instagram. Kupitia kampeni hiyo mteja anaebashiri kwa usahihi matokeo ya mechi ya siku husika hupata fursa ya kujishindia kifurushi cha Mambo pamoja na cha michezo cha Sports Plus cha jumla ya shilingi 36,000/-.”
“Mbali na hapo pia kuna zawadi zingine zinazotokana na kampeni ya hashtag ya #CopaAmericaonStarTimes kupitia mitandao yetu pia. Mshindi wa kampeni hii hupatikana kwa kushea mara nyingi zaidi post atakayoiona kuwekwa na kurasa za StarTimes na kufikia watu wengi zaidi. Mshindi wa kwanza wa kampeni atapatiwa tiketi VIP ya kwenda ya kwenda Ujerumani kutazama mechi za Bundesliga msimu ujao pamoja na dola za Kimarekani 1500/-, huku wa pili na wa tatu watapatiwa simu za mkononi za kisasa aina ya Solar 5. Tumefanya hivi ili kuwazawadia wateja wetu waaminifu na wanaofuatilia huduma zetu ili kunogesha zaidi shamra shamra za kombe la Copa America.” Alimalizia Bi. Hanif
Hatua ya robo fainali itakayoanza kupigwa kesho itazijumuisha timu zote zilizoshika nafasi ya pili katika makundi yao.
Wapenzi wa soka ulimwenguni wanazidi kusononeshwa na mwenedo mbovu wa kikosi cha taifa cha Brazil ambacho kimeshindwa kutinga hatua hiyo kwa kufanikiwa kushinda mechi moja tu kati ya tatu. Matokea hayo mabovu yamepelekea kocha wa taifa timu hiyo Dunga kutimuliwa kazi.
Timu na ratiba kwa timu zitakazopambana ni pamoja na Marekani na Ecuador (Juni 16), Peru na Colombia (Juni 17), na mechi za mwisho ni Argentina na Venezuela; Mexico na Chile (Juni 18). Timu zitakazopita hatua hii zitakutana katika hatua ya nusu fainali siku ya Juni 21.
0 Comments