Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jun 3, 2016

Rais wa Burundi awataka waasi kujisalimisha

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amewapatia waasi makataa ya wiki mbili kujisalimisha.''Iwapo hawatasalimu amri nitakabiliana nao kwa nguvu''.
Rais alitoa matamshi hayo wakati wa ziara yake katika mji wa Mugamba yapata kilomita 80 kusini mwa mji wa Bujumbura ambao umetajwa kuwa na makundi mengi ya waasi.

Ameonya kuwa vikosi vya usalama vitatumia mbinu kama hiyo zilizoangamiza maandamano dhidi ya serikali mwaka 2010 ambayo mashirika ya kibinaadamu yanasema yalihusisha unyanyasaji mkubwa.
Image copyrightGETTY
Image captionWanajeshi wa Burundi
Burundi imekabiliwa na ghasia za kisiasa za mda mrefu tangu rais Pierre Nkurunziza kuamua kuwania muhula wa tatu mwaka uliopita.
Zaidi ya watu 400 wamefariki tangu kuanza kwa mgogoro huo mnamo mwezi Aprili 2015 na takriban watu 260,000 wametoroka taifa hilo

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP