Habari

Dar es Salaam, Juni 02, 2016- Kampuni
ya Tigo Tanzania leo  imetangaza ofa mpya ambayo watumiaji wote wa
simu ambazo ni bandia  watapata simu halisi kila  watakapotembelea
duka la huduma kwa wateja la Tigo kubadilishwa simu hizo.


Mradi huu  unalenga kuwawezesha
Watanzania kupata simu halisi kutokana na ukomo wa matumizi ya
simu  kwa wale walio na simu feki unafikia  mwisho wake.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Mamlaka ya Usimamizi wa
Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitangaza kuwa  simu zote
bandia  na ambazo sio za viwango vinavyokubalika  ambazo
ziko katika soko la Tanzania  zitazimwa kuanzia Juni 16 mwaka huu.

Akitangaza ofa hiyo Mkuu wa Vifaa wa Tigo, David
Zakaria  alisema kuwa kampeni hiyo ya utambuzi imo katika mkakati wa
kampuni katika kuisaidia mikakati ya serikali  pamoja na Watanzania  dhidi
ya bidhaa bandia  na hali kadhalika  kukidhi usalama wa
mifumo ya malipo ya Tigo Pesa.

Akifafanua kuhusu ofa hiyo
kwamba  kimsingi inawalenga  wateja walio na simu bandia
Zakaria alisema, “Tunawataka wateja wetu kutembelea maduka Tigo ya huduma kwa
wateja  yaliyopo nchi nzima kuhakiki simu zao na baada ya kuhakiki,
wote wataobainika kuwa na simu feki watapata simu halisi aina ya Itel 2100
watakaponunua kifurushi cha 22,000/-.



Zakaria alisema
ofa hiyo ni nono kwani kwa kawaida, simu hiyo huwa inauzwa kwa bei ya 30,000/-
na sasa itapatikani kwa 22,000/- tu, huku akiongeza kuwa simu hiyo itakuwa na
dakika 350 za kupiga simu bure katika mitandao yote, ujumbe wa maneno 1,000 na
MB250 za intaneti kila mwezi kwa miezi mitatu.