Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jun 21, 2016

Trump amtimua meneja kampeni wake

Mgombea urais nchini Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican,Donald Trump, amemtimua kazi meneja kampeni wake.Corey Lewandowski ni mfuasi wa bwana Trump tangu alipotangaza nia ya kugombea urais na kupata ridhaa ya chama chake, kuchaguliwa kuwa mgombea rasmi nchini humo.

Lakini mwandishi wa BBC aliyeko mjini Washington anasema kwamba bwana Lewandowski amekuwa katika wakati mgumu wa kupambana na timu mpya iliyoajiriwa hivi karibuni na Donald Trump kwa lengo la kuweka sawa oparesheni zake kuelekea uchaguzi mkuu.
Mwandishi wa BBC,anaendelea kueleza kwamba nao wanachama wa Republican siku za hivi karibuni wamekuwa na wasiwasi juu ya matamshi ya Trump hasa alipozungumzia mauaji yaliyotokea mjini Orlando kwamba yanaweza kupunguz aidadi ya wapiga kura.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP