Mashirika matatu ya umoja wa mataifa yameonya kuwa Sudan Kusini inakumbwa na viwango vya juu uhaba wa chakula.
Karibu watu milioni tano watakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula wiki chache zinazokuja kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Afisa mmoja wa cheo cha juu wa Umoja wa Mataifa, amesema kuwa ni suala la kushangaza kuwa uhaba wa chakula umeathiri hata yale maeneo ambayo hayakukumbwa na mapigano.
Tangu mwanzo wa mwaka huu zaidi ya watoto 100,000 wametibiwa utapiamlo