Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Jun 15, 2016

Wafukuzwa shule baada ya picha za Nkurunziza kuharibiwa

Zaidi ya wanafunzi 200 nchini Burundi wamefukuzwa kutoka taasisi za elimu baada ya picha za rais Pierre Nkurunziza kuharibiwa.
Maafisa walisema kuwa wanafunzi katika eneo la Gahinga mashariki mwa nchi, waliadhibiwa kwa kukataa kumfichua yule aliyetekeleza kitendo hicho.

Mapema mwezi huu, watoto wa shule 6 ni kati ya watu waliokamatwa kwa madai kuwa waliharibu picha za rais zilizo katika vitabu vya shule vya kusoma.
Burundi imekumbwa na ghasia tangu bwana Nkurunziza kuwania na kushinda urais kwa muhula wa tatu mwaka uliopita.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP