Na Leonard Msigwa/GPL
WANAMUZIKI wawili maarufu nchini Ali Kiba na Baraka Da Prince wanaosimamiwa na lebo ya Rockstar 4000 jana Julai 20, 2016 walivamiwa na majambazi saa tatu usiku kwa saa za Afrika Mashariki wakiwa safarini nchini Afrika Kusini.
Managementi inayowasimamia wasanii hao ya Rockstar 4000 imesema wasanii hao walivamiwa wakiwa kwenye kikao cha mikakati ya kuzungumzia safari yao nchini humo watakakokaa kwa muda wa siku saba.
Chanzo hicho kimesema majambazi hao walikuwa na silaha za moto (bunduki).
Miongoni mwa vitu walivyoibiwa ni pamoja na simu zao za mkononi ambapo majambazi hao wakati wote wa tukio waliwanyooshea bunduki kina Ali Kiba kuwatisha zaidi na bila kutaka kupoteza muda.
Baraka Da Prince na Ali Kiba wote ni wazima wa afya na hawakudhurika kwenye hilo tukio.
Pamoja na tukio hili kutokea, wasanii hao hawatorudi nchini bali wataendelea na mipango yao iliyowapeleka nchini humo.
0 Comments