Msanii Jacqueline Wolper.
Msanii wa filamu za Kitanzania ambaye anajulikana kwa kazi zake nzuri za uigizaji Jacqueline Wolper usiku huu mjini Dodoma ameutangazia umma kwamba amerudi tena kwenye Chama cha Mapinduzi.Wolper ambaye mwishoni mwa mwa jana alijipatia umaarufu mkubwa sana pale alipokihama chama cha Mapinduzi na kuwa bege kwa bega na chama cha Chadema.Akieleza kwa kifupi mapenzi yake kwa aliyekuwa Rais wa awamu ya nne Mheshimiwa Jakaya Kikwete,Wolper alisema kwamba alikuwa akimpenda sana Rais Kikwete na amemtakia heri katika safari yake ya mapumziko kikazi.

Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amemkaribisha Wolper kwa mikono miwili.