Jana ilikuwa siku maalumu kwa ndugu Hamza na mkewe mama Hajra baada ya kutoa mualiko wa Iftar kwa ndugu na jamaa  nyumbani kwake Herentals kitongoji kidogo kilichopo nje ya jiji la Antwerpen nchini Ubelgiji.Pichani baadhi ya waumini waliohudhuria Iftar hapo jana
Kamanda wa makamanda mtaalamu wa misitu {mwenye shati la drafti} akitoa mawaidha kuhusiana na Upendo baina ya rafiki kwa rafiki,husda baina ya rafiki na rafiki na kinga za kujilinda na urafiki mbaya hapo jana,Baadhi ya waumini wakimsikiliza kwa makini Kamanda huyo.

Kwa upande wa kina baba wakipata sadaka ya Iftar nyumbani kwa Hamza na mkewe mama Hajra
Kina baba wakiendelea na sadaka ya Iftar hapo jana 
Kwa upande wa kina mama hawa ni baadhi ya waliohudhuria kuftari pamoja nyumbani kwa bwana Hamza na mkewe mama Hajra kitongojini Herentals nchini Ubelgiji
Dada yetu Malika kutoka Liege pia alihudhuria Futari ya pamoja hapo jana
Malika akiwa na watoto wake wakiendelea na Iftar 
Kina baba wakiendelea kupata sadaka ya Futar  iliyoandaliwa na Hamza na mkewe hapo jana
Baada ya futar kila mmoja alikuwa na furaha ya kumsikiliza mtaalamu wa misitu Kamanda wa Makamanda,pichani Kamanda akifurahisha waumini kwa darsa la mawaidha ya kuelimishana juu ya upendo dhidi yetu
Darsa likiendelea huku waumini wakiwa makini kabisa kumsikiliza Kamanda ambaye hayupo pichani
Mwenyeji wa shughuli ambaye ndiye baba mwenye nyumba bwana Hamza{aliyekalia miguu} akiwa makini kumsikiliza mtaalamu wa misitu jana wakati akitoa darsa nyumbani kwake baada ya Iftar.Hamza na mkewe jana walitoa sadaka ya Futar kwa waumini wenzao waliofika nyumbani kwake Herentals.
Mama mwenye nyumba ambaye ndiye mke wa Hamza,mama Hajra akitoa shukrani za dhati kwa kina mama waliofika nyumbani kwake kwa kujumuika pamoja katika Iftar iliyoandaliwa na yeye na mumewe katika kitongoji cha Herentals nje kidogo ya jiji la Antwerpen.{Picha na maelezo toka Maganga One Blog}.