Mchezo wa tatu wa robo fainali ya Uefa Euro 2016 kati ya Ujerumani na Italia uliochezwa usiku wa kuamkia leo umemalizika kwa Ujerumani kufuzu nusu fainali ya michuano hiyo.
Katika robo fainali hiyo ambayo kwa dakika 120 ulimalizika kwa sare ya goli 1-1, goli la Ujerumani likifungwa na Mesut Ozili dakika ya 65 kisha Italia kurudisha goli hilo katika dakika ya 78 kupitia mkwaju wa penati uliopigwa na Leonardo Bonucci.

Baada ya sare hiyo waliingia katika hatua ya mikwaju ya penati ambapo kwa upande wa Ujerumani waliopata ni Toni Kroos, Julian Draxler, Mats Hummels, Joshua Kimmich, Jerome Boateng na Jonas Hector na waliokosa ni Thomas Muller, Mesut Ozil na Bastian Schweinsteiger.
Kwa upande wa Italia waliopata ni Lorenzio Insigne, Andrea Barzagli, Emmanuel Giaccherini, Marco Parolo na Mattia De Sciglio na waliokosa ni Simone Zaza, Graziano Pelle, Leonardo Bonucci na Matteo Darmian