Mbunge wa jimbo la Madaba mkoani Ruvuma, Joseph Mhagama (wa tatu kulia) akipokea moja ya madawati 540 kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha cha 842 KJ Mlale Meja Absolomon Lyanga Shaushi kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa madawati kwa shule za msingi na sekondari katika jimbo hilo.

Mkuu wa kikosi cha 842 KJ Mlale kilichopo wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, Meja Absolomon Shaushi (kushoto) akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Madaba wilayani Songea, Joseph Mhagama (kulia) mara baada ya kukabidhi madawati 540 ili kukabilianana upungufu wa madawati katika jimbo hilo.

Mkuu wa Kikosi cha cha 842 KJ Mlale Meja Absolomon Lyanga Shaushi akimuonesha Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Songea, Mennas Komba (kulia), baadhi ya madawati yaliyotengenezwa na kikosi hicho ambayo yatasambazwa kwa baadhi ya shule za msingi na sekonadri zenye upungufu wa madawati. katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Simon Bulenganija.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini ambaye pia ni Katibu wa Mbunge wa jimbo la Peramiho Jenista Mhagama, Mennas Komba (kulia) akipokea moja ya madawati 534 kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha cha 842 KJ Mlale Meja Absolomon Lyanga Shaushi, ambayo yametengenezwa na kikosi hicho ili kukabiliana na upungufu wa madawati katika jimbo la Peramiho,katikati mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilayaya Songea vijijini Simon Bulenganija.

Picha na Muhidin Amri