Mbunge
wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso katika akipongezwa na wananchi wa
Jimbo la Pangani mara baada ya kutangazwa na Mahakama Kuu Kanda ya Tanga
kuwa mshindi halali katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba mwaka
jana
mara
baada ya kuonekana hakuna vigezo vya kutengua matokeo hayo katika kesi
ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CUF Amina
Mwidau







Mbunge
Aweso Jumaa akiwa amebebwa juu juu na wananchi wa Jimbo la Pangani mara
baada ya kesi iliyofunguliwa dhidi ya mpinzania wake wa CUF Amina
Mwidau ya kupinga matokeo ya uchaguzi kutupiliwa mbali na mahakama kuu
kanda ya Tanga




MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tanga jana
imetupilia mbali shauri la kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Pangani
lililofunguliwa na aliyekuwa mgombea kupitia tiketi ya  CUF Amina
Mwindau dhidi ya Mbunge wa Jimbo hilo Jumaa Hamidu Aweso CCM  na
kuonekana hakuna vigezo vya kutengua matokeo hayo.



Akizungumza wakati akitoa huduma ya Shauri hilo,Jaji Patricia Fikirini
alisema mlalamikaji Amina Mwindau CUF ameonekana kushindwa katika shauri
hilo dhidi ya mlalamikiwa Jumaa Aweso katika upingaji wa matokeo ya
uchaguzi mkuu uliofanyika oct  25 mwaka jana.



Alisema miongoni mwa malalamiko yalioambatanishwa kutoka kwa

mlalamikaji katika zoezi zima la kupinga matokeo hayo ni pamoja na kuwa
mlalamikiwa ambae ni Jumaa Aweso katika kampeni zake alikiuka taratibu
za uchaguzi,ubaguzi wa mgombea wa jinsia ya kike na kutumia lugha ya
siziokuwa za kiungwana jambo ambalo mlalamikaji alidai lilimgharimu
kupata matokeo mazuri katika uchaguzi huo.



Alisema sambamba na vielelezo vilivyoletwa mahakamani hapo pamoja na
ushahidi uliotolewa kwa upande wa mlalamikaji havikuwa na ushawishi wa
kuweza kutengua matokeo ya uchaguzi huo.



Jaji Fikirini alisema amezingatia hoja zote kutoka pande mbili na

kujiridhisha Jumaa Aweso ambae ni mbunge hivi sasa kuwa ni mbunge
aliyepita kihalali na hakukuwa na vigezo vya upingwaji wa matokeo
aliyopata katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.



Alisema haki zote za kisheria zipo wazi kwa pande zote mbili

mlalamikiwa na mlalamikaji ikiwa pamoja na kukata rufaa kwa maamuzi
yaliyochukuliwa na Mahakam hiyo ikiwa kama kuna upande hauta ridhika na
hukumu iliyotolewa.



Kwa upande wake  Wakili wa kujitegemea na mahakama kuu Warehema Kibaha
alisema Jaji Patisia Fikirini amefanya maamuzi sahihi ya kutenda haki
kwa mteja wake katika shauri hilo lililo dumu kwa takriban miezi
7.



Wakili Kibaha alisema katika shauri hilo walijiandaa kwa ushahidi  na
mashahidi wazuri ili kuweza kukabiliana na kesi hiyo jambo
ambaloliliwawezesha kupata ushindi wa kihalali na kuweza kumpa nafasi
mteja

wake kuendelea na majukumu yake ya Kibunge.



Nae Wakili Mashaka Ngole aliyemsimamia Mlalamikaji Amina Mwindau alisema
hana pingamizi lolote na  atamsikiliza mteja wake ikiwa ataamua kukata
rufaa wataangalia vigezo muhimu vitakavyo wasaidia katika awamu ya pili
pindi watakapo kata rufaa hiyo



Mbunge wa Jimbo la Pangani Jumaa Aweso ambaye alikuwa anakabiliwa katika
shauri hilo alisema kipindi chote alichokuwa anakabiliana na kesi hiyo
kulimpotezea umakinifu wa kufanya majukumu yake ya kibunge na kuweza
kuangalia shida za wananchi wa Pangani kwa umakini zaidi.



Aweso alisema kesi imekwisha na sasa kilichombele yake ni kupambana na
kero za wananchi wa Wilaya hiyo ili kuweza kuwaletea maendelo kama
alivyowaahidi kipindi cha kampeni.
 
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha