DAR ES SALAAM: Mbunifu wa mitindo mbalimbali ya nguo kama ‘Kwachukwachu’ na nyingine, Martin Kadinda ambaye pia ni meneja wa staa mwenye nyota kali Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, inaonesha kibarua hicho kimeota mbawa na nyuma yake kuna mazito.
YASEMEKANA HAJAFANYA CHOCHOTE KWA WEMA
Habari ambazo zimenyetishwa kutoka familia ya akina Wema zinadai kuwa walikuwa wanakereka na aina ya umeneja anaouendesha Kadinda katika kampuni ya Wema ya Endless Fame na kwamba mara nyingi walikuwa wakiona kuwa yeye ndiye anajinufaisha zaidi kuliko Wema katika nyanja zote za kuingiza kipato.
MAMA AAMUA AINGILIA KATI
Kufuatia hali hiyo, mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu ndipo akaamua kumtimua Kadinda na kuwa mstari wa mbele kusimamia vitu vyake na kusema kuwa amechoshwa na watu kumtumia mtoto wake kwa manufaa yao wenyewe.
“Ni hivi, mimi ni mama, najua uchungu wa mtoto wangu na kila kitu kinachomuhusu, naumia kuona watu wanatumia jina la mwanangu lakini yeye anabaki bila kitu, sasa nimesema inatosha, sasa hivi nimeamua kumsimamia mtoto wangu mwenyewe kwa kila kitu,” alisema.
AMBUNIA VIATU
Mama huyo ambaye kwa muda mchache alioamua kuingilia kati kumsimamia mtoto wake, tayari ameshambunia mtoto wake huyo viatu aina ‘sandozi’ yenye jina la mtoto wake huyo na sasa vinauzwa mitaani.
“Nimeamua nianze na viatu na vitu vingi sana vinakuja na namshukuru Mungu viatu vimeanza kufanya vizuri sana sokoni,” alisema mama Wema.
VIPI KUHUSU KUMTUMBUA KADINDA?
Baada ya kufunguka hayo, Amani lilimbana mama huyo kuhusu nafasi ya Kadinda kwa kuwa inaonekana kama ameichukua yeye kwa sasa kwa kuamua kumsimamia mtoto wake kwa kila kitu
“Nimeamua kumsimamia mtoto wangu lakini kuhusu hayo mambo mengine sijui kwa kweli,” alisema mama huyo.
KADINDA HUYU HAPA
Amani pia lilipomaliza kuzungumza na mama Wema lilimvutia waya Kadinda aliyejitetea kwa kusema kuwa yuko nje ya nchi atakaporudi atalizungumzia suala hilo vizuri.
“Naomba unipe muda kidogo narudi na ndiyo nitaweza kukaa na kuzungumza na wewe vizuri kuhusu hilo bila tatizo,” alisema Kadinda.
Baada ya kumaliza kuzungumza na wote hao Amani bado likamtafuta Wema, mwenyewe kuzungumzia kizungumkuti hicho cha kumuengua Kadinda kumsimamia vitu vyake kama meneja.
Amani: Eti kuna tetesi kuwa Kadinda siyo meneja wako tena na kwamba mama yako ni kila kitu kwa sasa, je, ni kweli?
Wema: Aisee kuna habari nyingine huwa ni ngumu kujibu.
Amani: Kwa nini?
Wema: Huwa ipo hivyo kwa sababu hakuna sehemu niliyowahi kuzungumza kwamba Kadinda siyo meneja wangu tena.
Amani: Kwa sababu sasa hivi mama anaonekana kushika usukani kwa kila kitu?
Wema: Kwani mama akishika usukani kuna tatizo gani? Ni mama na yeye pia ana nafasi kwangu tena kubwa sana. Pia Kadinda ana nafasi yake
0 Comments