Nigeria imetia saini mkataba wa mafuta na nchi ya China wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 80. Kampuni ya mafuta nchini humo imesema kuwa kiasi cha fedha kitatumika kuimarisha viwanda vya ndani.

Licha ya kuwa miongoni kwa nchi za Afrika zinazozalisha mafuta kwa kiasi kikubwa,Nigeria inaingiza kiasi kikubwa cha mafuta kutoka nje kutokana na viwanda vyake vingi kutufanya kazi.
Nchi hiyo pia inakabiliwa na mashambulizi ya wanamgambo ikiwemo Boko Haram wanaotaka kupata sehemu kubwa ya utajiri wa mafuta.