Rais wa Marekani Barack Obama amemsifu sana mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton na kusema ndiye afaaye zaidi kuongoza Marekani.
Akihutubu katika kongamano kuu la chama cha Democratic mjini Philadelphia, huku akishangiliwa na wajumbe, Rais Obama amesema hakujawahi kuwa na mtu aliyehitimu zaidi kuongoza Marekani kuliko Bi Clinton.
"Hakujawahi kuwa na mwanamume au mwanamke, iwe mimi au Bill Clinton au mtu mwingine yeyote aliyekuwa amehitimu zaidi kuwa rais kama yeye," amesema Bw Obama.
Amemsifu pia kwa kujikakamua na kuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya taifa hilo kuteuliwa kuwa mgombea urais wa chama kikubwa.

ObamaImage copyrightGETTY
Image captionObama ameshutumu sera za Donald Trump

Amempongeza kwa kubomoa vizuizi na kuunda nafasi zaidi kwa Wamarekani.
Amewaahidi Wamarekani kwamba Bi Clinton anatetea umoja na maadili ya Wamarekani.
Bw Obama pia amemkosoa vikali mgombea wa chama cha Republican Donald Trump.
Awali, Seneta wa Virginia Tim Kaine alikubali rais uteuzi wa kuwa mgombea mwenza wa Bi Clinton