Mamlaka ya Uturuki imesema kuwa itazichukua shule na hospitali mjini Mogadishu ambazo zilikuwa zikiendeshwa na shirika linalohusishwa na jaribio la mapinduzi la hivi majuzi dhidi ya rais Recep Erdgan.
Serikali ya Somalia wikiendi iliagiza wafanyikazi wote wa vuguvu la Gulen kuondoka Mogadishu.
Hatua hiyo imesababisha,operesheni zake kusitishwa katika shule na hospitali , na hivyobasi kuhatarisha maisha ya wagonjwa huku mashine ya kipekee ya kusafisha damu mjini Mogadishu ikiwa haifanyi kazi.

Image captionHospitali nchini Somalia

Hatua hiyo ya serikali ya Somalia ya kufunga huduma zinazoendeshwa na Nile Academy mjini Mogadishu ,ilikuwa ya haraka lakini ilitarajiwa.
Nile Academy inayohusishwa na Fathellah Gulen ilikuwa ikiendesha shule na hospitali mjini Mogadishu,lakini serikali ya Somalia ni mshirika wa karibu wa rais wa Uturuki Recep Tayyeb Erdogan.
Shule zilizoathirika kwa sasa hazina watu kufuatia kuondoka kwa wafanyikazi wote kutoka Uturuki.

Image captionShule nchini Somalia

Hopsitali ilioathirika zaidi ni ile ya Deva ambayo ilikuwa ikitoa huduma muhimu kama vile usafishaji damu wa wagonjwa wa figo.
Madaktari katika hopsitali hiyo wamesema kuwa wanawahudumia zaidi ya wagonjwa 60 wa figo kila siku,ambao hawana pa kukimbilia.