Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusu kuwepo kwa hali mbaya ya kibinaadam nchini Sudan kusini , maelfu ya watu wakiyakimbia makazi yao kutokana na machafuko.Shirika la kuhudumia wakimbizi linasema Njaa na maradhi vinatishia maisha ya maelfu ya watu ambao wamebaki nchini humo.
Makundi ya watu wenye silaha pia yamewazuia watu wengi kuingia nchi jirani ya Uganda na kuna ripoti ya kuwepo na vitendo vya watoto kusajiliwa kwa nguvu kwenye jeshi.Upungufu mkubwa wa chakula na mlipuko wa maradhi ya kipindupindu umefanya hali kuwa mbaya zaidi.

Image copyright

Mpango wa kumaliza mapigano kati ya Serikali ya Rais Salva Kiir na mpinzani wake mkubwa Riek Machar ulivunjika mwezi uliopita.Katibu mkuu wa masuala ya kibinaadam wa umoja wa Mataifa, Stephen Obrien amesema mahitaji ya Sudani kusini ni Changamoto kubwa ''tunaweza kushuhudia , watu wengi wengi wanahitaji huduma, wanahitaji kusaidiwa, lakini zaidi wahitaji kulindwa.
Hivyo tunahitaji si tu kutazama maeneo yanayozunguka kambi hapa, lakini tunapaswa kutazama nje pia na kufikiria namna gani wau hawa watalindwa dhidi ya machafuko. Hasa wanaoathirika ni watoto na wanawake, wagonjwa na walemavu wanaohitaji msaada, hiyo ni changamoto kubwa tunayopaswa kuikabili''