Rais anayetetea kiti chake nchini Gabon, Ali Bongo na mpinzani wake mkuu Jean Ping, kila mmoja amedai ushindi, kufuatia uchaguzi wa Rais uliofanyika nchini humo Jumamosi.

Rais Ali Bongo akiwa katika kampeni nchini Gabon
Image captionRais Ali Bongo akiwa katika kampeni nchini Gabon

Pande zote zimekuwa zikilaumiana kwa udanganyifu. Jean Ping amewaambia wafuasi wake kwamba ameshinda uchaguzi huo na anamsuburi Rais anayemaliza muda wake kumpongeza. Na kwa upande wa timu ya Rais Bongo imesema inaendelea na awamu nyengine madarakani.
Kufuatia mvutano huo wa pande hizo mbili, Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo amearifu kuwa si halali kwa mtu yoyote kutangaza matokeo, isipokuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi pekee ndiyo yenye wajibu wa kufanya hivyo.

Jean Ping,mpinzani wa Rais Ali Bongo
Image captionJean Ping,mpinzani wa Rais Ali Bongo

Jean Ping, kiongozi wa zamani katika Umoja wa Afrika anajaribu kuuondoa madarakani utawala wa Bongo ambao umekaa madarakani kwa karibu miaka 50.