TAKWIMU
zilizotolewa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Twaweza imeonyesha kuwa
asilimia 96 ya wananchi wanakubali hatua za kiutendaji kazi za Rais John
Pombe Magufuli ikiwemo uondoaji wa wafanyakazi hewa na sera ya elimu
bure.

Taarifa iliyotolewa leo katika vyombo vya habari na Mshauri
Mwandamizi wa Mawasiliano wa Twaweza, Risha Chande alisema asilimia 88
ya wananchi wana imani kuwa Rais Magufuli ataendelea na kasi aliyoanza
nayo mpaka mwisho wa awamu yake ya kwanza ya uongozi.



“Utafiti
huu unaonyesha kuwa asilimia 69 ya wananchi walifuraishwa na juhudi za
Rais za uondoaji wa wafanyakazi hewa, wakati asilimia 61 walipongeza
sera ya elimu bure wakati asilimia 61 walifurahishwa na usimamishwaji wa
watumishi wa serikali” alisema Chande.

Chande alisema kuwa
katika utafiti huo unaonyesha wananchi wengi kuridhishwa na hatua
zilizochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano ya kufanya maboresho katika
huduma za umma ikiwemo mamlaka ya mapat (asilimia 85), mashuleni
(asilimia 75),vituo vya polisi (asilimia 74),mahakama (asilimia 73),
vituo vya afya (asilimia 72).

Aliongeza kuwa kwa upande wa
huduma zinazotolewa katika utumishi wa umma, utafiti unaonyesha kuwa
asilimia 95 ya wananchi wanaridhishwa na huduma zinazotolewa na
madaktari, walimu, na maofisa tawala katika ofisi za umma.

“Pamoja
na kiwango kikubwa cha kukubalika kwa Serikali ya wamu ya Tano wananchi
wamesema suala la umakini na kanuni za demokrasia na haki ni vyema
zifuatwe ambapo wananchi nane kati ya kumi wanasema watendaji
waondolewe pale tu panapokuwepo udhibitisho wa vitendo viovu” alisema
Chande.

Akifafanua zaidi Chande alisema utafiti huo pia
umeonyesha kubadilika kwa matarajio ya wananchi ambapo katika kipindi
cha nyuma kulikuwa na hali ya kutojali miongoni mwa wananchi
kulikotokana na utendaji duni kutoka kwa watendaji