Wanajimu katika maeneo tofauti ya bara Afrika wameona moto wa mviringo angani wakati wa kupatwa kwa jua.
Jua hupatwa wakati ambapo mwezi huwa mbali na dunia ikilinganishwa na wakati jua linapopatwa kabisa.

Kupatwa kwa jua
Image captionKupatwa kwa jua

Matokeo yake huwa ni mviringo mkubwa unaong'aa ukiwa umezunguka eneo jeusi .
Picha nzuri ni zile zilizoonekana nchini Tanzania ambapo tukio hilo lilichukua mda wa dakika tatu.
Kupatwa huko kwa jua pia kulionekana nchini Gabon,Congo-Brazaville,DRC Madagascar na kisiwa cha Re-union.

watu wakitumia kila njia kuona jua linavyozibwa
Image captionwatu wakitumia kila njia kuona jua linavyozibwa

Wakati ambapo mwezi uko mbali na dunia ,huonekana mdogo na hauwezi kuliziba jua kabisa wakati wa kupatwa kwa jua.Matokeo yake hujulikana kama mviringo wa moto.
Kupatwa kwengine kwa jua kunatarajiwa kufanyika mnamo mwezi Februari 2017 na huenda kukaonekana katika maeneo ya Marekani kusini na Africa.