KIWANDA
CHA SARUJI CHAIPIGA TAFU SHULE YA SEKONDARI YA ILBORU YA ARUSHA



Tanga,
KIWANDA
Cha Saruji Cha Simba (Simba Cement) cha Tanga, kimeipa shule ya Sekondari ya
Ilboru Secondary School ya Arusha mifuko 400 ya saruji yenye thamani zaidi ya
milioni 4.8 kwa ujenzi wa vymba vya madarasa.



Akizungumza wakati wa
halfa fupi ya
makabidhiano leo, Mkuu wa Idara ya Rasilimaliwatu kiwanda cha Saruji cha Simba
Cement, Diana Malambugi, alisema msaada huo umetolewa ili kupunguza changamoto
za vyumba vya madarasa kwa shule hiyo.


Alisema msaada huo
utapunguza uhaba
wa vyumba vya madarasa na kutoa wito kutumika kama ilivyokusudiwa na kuiagiza
kamati ya shule kuhakikisha mifuko hiyo inatumika
ipasavyo.


‘Mifuko hii ya saruji
itapunguza changamoto
inayoikabili shule yako  ikiwemo vyumba
vya madarasa na ujenzi wa nyumba za walimu, sera yetu moja wapo ni hii ya elimu”
alisema Malambugi


Alimtaka mwalimu huyo
na kamati yake
ya shule kuitunza mifuko hiyo ya saruji na kumhakikishia kuisaidia pale ambapo
kutakuwa na uhitaji na kuwataka wadau wengine wa elimu kusaidia sekta ya elimu
zikiwemo kuondosha changamoto za uhaba wa madawati na vyumba vya
madarasa.


Kwa upande wake,
mwalimu mkuu wa
shule ya Ilboru sekondari school ,  Julias
Shulla, alikishukuru kiwanda hicho na kusema kuwa msaada huo utatumika kama
ilivyoombwa.


Alisema shule yake
inakabiliana na
changamoto nyingi zikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja uhaba wa vifaa
vya maabara hivyo kuwataka wadau wa elimu
kuisaidia.


‘Tunakishukuru kiwanda
cha saruji
cha simba kwa moyo wao waliounyesha kwetu, kwa fadhila hii tunawaahidi kuwa
tutaitumia saruji kama tulivyoiomba” alisema
Shulla


Alisema mifuko hiyo
itapunguza kwa
kiasi kikubwa  changamoto ambazo shule
yake inakabiliana nazo na kusema kuwa msaada huo ni faraja kwao na wanafunzi wa
shule yake.



                                                     
Mwisho















Mkuu wa Idara ya
Rasilimawatu
kiwanda cha Sauji cha Simba Cement cha Tanga, Diana Malambugi,
akimkabidhi mifuko
ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya milioni 4.8 kwa mwalimu mkuu shule ya
Sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla  ikiwa
ni ujenzi wa vyumba vya madarasa.nyuma
kulia ni Mkuu wa fedha Pieter Jaggar na kushoto ni Emmanuel Jonas
mhasibu.























  Mhasibu wa kiwanda cha
Saruji cha Simba Cement, Emmanuel Jonas, akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya
Sekondari ya Iboru ya Arusha, Julias Shulla mifuko ya saruji 400 yenye thamani
zaidi ya shilingi milioni 4.8 kwa ajili ya ujenzi wa vymba vya madarasa, nyuma
ni mkuu wa fedha, Pieter Jaggar.



















 Afisa Uhusiano kiwanda
cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga, Mtanga Nnour, akimkabidhi mifuko ya
saruji 400 yenye thamani zaidi ya shlingi milioni 4.8 kwa
mwalimu  mkuu wa shule ya sekondari ya Ilboru ya
Arusha, Julias Shulla, ikiwa ni kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa. Nyuma
ni mkuu wa fedha, Pietre Jaggar.











 Mkuu wa fedha kiwanda cha
saruji cha Simba Cement, Pieter Jaggar, akimabidhi mifuko ya saruji 400 yenye
thamani zaidi ya shilingi milioni 4.8 mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya
Ilboru ya Arusha, Julias Shulla ikiwa ni kusaidia ujenzi wa vyumba vya
madarasa, kulia ni meneja usambazaji na ugawaji, Samwel Shoo, nyuma kulia ni
Afisa Uhusiano , Nour Mtanga  na mkuu wa
Idara ya Rasilimawatu, Diana Malambugi.


Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Kumekucha.
0655902929