Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akiandika baadhi ya hoja kutoka kwa baadhi ya wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba inayotarajiwa  kufanyika
siku ya jumatano
tarehe 07 /09 /2016 na alhamisi tarehe 08 /09 /2016.

baadhi ya wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi.



Na fredy mgunda,ileje

Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi, amewaasa wasimamizi wa mitihani ya
kumaliza elimu ya msingi kutofanya kazi kwa mazoea ili kutoruhusu mianya
itakayowafanya wanafunzi wasiokuwa na uelewa kufaulu mitihani hiyo.
Alisema kumekuwa na baadhi
ya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika wanafaulu mithani hiyo kitendo
kinachotia mashaka kwa wasimamizi hao kushindwa kunyakazi waliyopewa kwa makini.

Mnasi aliyasema hayo jana, wakati
akitoa semina ya mafunzo kwa wasimamizi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje ambapo
alisema usimamizi hafifu wa mitihani umesababisha kuwepo kwa watumishi
wasiokuwa na uwezo kitaaluma.

Aidha kabla ya uteuzi wa Rais wa jamhuri ya muungazo wa tanzania Dr John Pombe Magufuli mkurugenzi huyo ambaye
kitaaluma ni mwalimu alikuwa afisa elimu shule ya msingi manispaa ya iringa alisema
iwapo ikibainika kufaulu kwa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika mtuhumiwa wa
kwanza kwenye uzembe huo atakuwa msimamizi wa mitihani na hatua kali
zitachukuliwa zidi yake.
“Nawatahadharisha kwamba
mnaweza mkarubuniwa kuwawezesha wanafunzi wasiokuwa na sifa wafaulu mitihani hiyo,kufanya
hivyo ni kukiuka kanuni za usimamizi na uendeshaji wa mtihani na kuwaambia
hayupo tayari kutumbuliwa na rais kwasababu za wasimamizi”alisisitiza
Mnasi.
Hata hivyo Mnasi aliwataka
wasimamizi hao kuwa makini katika kufanyakazi hiyo na kama kuna jambo lolote
ambalo hawajalielewa kuhusu kazi hiyo ni vyema wakauliza ili kupewa majibu.
“hakikisheni kuwa taratibu
zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo na kuwataka wasimamizi wote kufanya
kazi yao kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu.“Nawaasa wasimamizi  wa mitihani kujiepusha na vitendo vya udanganyifu
kwani serikali itachukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kukiuka taratibu
za mitihani,” alisema
Mnasi.

Mnasi alibainisha kuwa,
serikali imezingatia uwezo wa kitaaluma, uadilifu na uaminifu hivyo wasimamizi
hao kupewa jukumu la kusimamia mitihani hiyo muhimu ya kitaifa.

Aliongeza kuwa mitihani hiyo
ni muhimu ili kuliwezesha taifa kupima kiwango cha elimu kilichpo nchini na
kuwapata wasomi wa kiwango cha juu.

Nao wasimamizi wa mitihani
hiyo wamemuahidi mkurugenzi huyo kuwa watasimamia mitihani hiyo kwa kufuata sheria
na kanuni za usimamizi wa mitihani walizopewa.
Lakini mitihani hiyo ya
kuhitimu darasa la saba inatarajiwa kufanyika siku ya jumatano
tarehe 07 /09 /2016 na alhamisi tarehe 08 /09 /2016.