MWENGE wa Uhuru baada ya kuwasili mkoani Singida Mwenge huu ni ni kitu mfano wa kikombe chenye mpini mrefu na utambi ambacho aghalabu
huwasha na kukimbizwa katika kusheherekea au kutukuza tukio fulani

Askari wa Jeshi la Polisi wakiulinda Mwenge ishara ya kuwasili muda mfupi kabla ya kukabidhi kwa uongozi wa Mkoa wa Singida




Kushoto ni Katibu
tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi
akimkabidhi Mwenge Mkuu
wa Wilaya ya Manyoni Mhe Geofrey Mwambe tayari kwa ajili ya kumulika Miradi 18 katika Wilaya hiyo




Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma walipowasili kukabidhi Mwenge katika Kijiji
cha Lusilile Kata ya Kintinku Wilaya ya Manyoni


Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwa ameushikia Mwenge ishara ya Makabidhiano mara baada ya kuwasili

Katibu
tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru
kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bi Rehema S. Madenge


 Wananchi wakishuhudia kwa karibu zoezi la makabidhiano ya Mwenge
Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Singida wakishuhudia zoezi la makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru
 Wengi wamefika kushuhudia Mwenge ukiwasili mkoani Singida
 Viongozi wa Mkoa wa Singida wakifanya mazoezi ya maandalizi ya kuupokea Mwenge
 Timiza wajibu wako kata Mnyoro wa Rushwa
Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi akisoma salamu za shukrani mara baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma katika Kijiji cha Lusilile



Na Mathias Canal, Singida



Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi leo ameupokea
Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bi Rehema S.
Madenge ambao utakimbizwa Mkoani Singida kwa siku saba katika
Halmashauri saba ambapo utaanzia Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.




Dkt Lutambi amekabidhiwa Mwenge huo pamoja na wakimbiza Mwenge Kitaifa
katika eneo la Kijiji cha Lusilile Kata ya Kintinku Wilaya ya Manyoni
ukiwa umewaka na kuahidi kuukabidhi kwa katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora
pasina mashaka utakapomaliza muda wake Mkoani Singida.



Lutambi
alisema kuwa mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani humo utalitia jumla ya miradi
61 inayohusu sekta ya ufugaji, Mazingira, Maji, Afya, Elimu, Barabara,
Utawala Bora, Kilimo, Ushirika, Biashara, Ardhi na Programu za mapambano
dhidi ya Dawa za kulevya, Malaria Rushwa na Ukimwi.



Alisema kuwa
jumla ya Miradi 33 itazinduliwa, 13 itawekwa jiwe la msingi minne
itawekwa jiwe la msingi na mingine mitano itatembelewa ambapo miradi
yote hiyo itakayopitiwa itakuwa na thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni
14.



Mbio za Mwenge wa uhuru kwa Mwaka 2016 zimebeba kauli mbiu ya
"Vijana ni nguvu kazi ya Taifa, Washirikishwe na kuwezeshwa" ambapo
hata hivyo kila Halamashauri nchini zimeelekezwa kutenga asilimia 5% ya
mapato yake ya ndani kwa ajili ya vijana na asilimia 5% nyingine kwa
ajili ya kina mama.



Katika kumaliza mizizi wa Rushwa, Dawa za
kulevya, ukimwi na Malaria Mwenge wa Uhuru umejikita zaidi katika kauli
mbiu ya "Timiza wajibu wako kata Mnyororo wa Rushwa" kwenye mapambano
dhidi ya Rushwa, Kauli mbiu ya "Tujenge jamii, Maisha na Utu wetu bila
dawa za kulevya" kwenye Mapambano dhidi ya Dawa za kulevya, Kauli mbiu
ya "Tanzania bila maambukizi mapya, Unyanyapaa na Vifo vitokanavyo na
UKIMWI inawezekana" kwenye Mapambano dhidi ya Ukimwi na Mapambano dhidi
ya Malaria, chini ya kauli mbiu ya " Wekeza katika maisha ya baadae,
Tokomeza Malaria".



Kwa upande wake katibu Tawala wa Mkoa wa
Dodoma Bi Rehema S. Madenge wakati akikabidhi Mwenge wa Uhuru Mkoani
Singida alisema kuwa Mwenge wa Uhuru umekimbizwa katika Wilaya zote saba
za Mkoa huo ambapo jumla ya Miradi 47 yenye thamani ya zaidi ya
Shilingi Bilioni 12.



Bi Madenge amewapongeza wananchi wote kwa
ushirikiano na juhudi kubwa walizofanya katika kuianzisha, kuiendeleza
na kuikamilisha Miradi yote.



Pia alisema kuwa katika Wilaya zote
walizozuru wakimbiza Mwenge wamepata taarifa za utekelezaji wa Ilani ya
uchaguzi ya Mwaka 2015 na kuelezea namna inavyoendelea kutekelezwa.




Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Geofrey Mwambe wakati
akikabidhiwa Mwenge wa uhuru na katibu Tawala wa Mkoa wa Singida amesema
kuwa Mwenge huo unataraji Kutembelea Miradi 18 ambapo hii leo
utatembelea miradi 7 na hapo kesho utatembelea Miradi 11.




Miongoni mwa Mirafi itakayofunguliwa ni pamoja na uzinduzi wa Programu
ya Ufuatiliaji na kuteketeza mbu, Kufungua Mradi wa ujenzi wa vyumba
viwili vya madarasa na matundu nane ya vyoo na ukarabati wa vyumba
viwili vya madarasa, Ufunguzi wa daraja la Makutupora, Kuzindua Klabu ya
wapinga Rushwa, Kuzindua Mradi wa Ujenzi wa kituo cha Maarifa ya
kupambana na UKIMWI, Kuzindua Mradi wa Vijana wa kufyatua matofali, na
Kuzindua Klabu ya Kupambana na Dawa za Kulevya.



Kwa mujibu wa
ratiba za mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka huu, unakimbizwa katika
Halmashauri na Manispaa zipatazo 179 na kilele cha mbio hizo ni Octoba
14 mwaka huu katika Mkoa wa Simiyu.



Mwenge wa Uhuru unaashiria
Nuru na Mwanga, Uliwashwa rasmi kwa mara ya awali juu ya kilele cha
Mlima Kilimanjaro Disemba 9, 1961