Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifungua  Mkutano Mkuu wa 14 wa Wahandisi katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam leo Septemba 1, 2016

Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe  Magufuli akipata picha ya  pamoja na Wanajeshi wa JWTZ Kikosi cha Anga  603 KJ Majumba Sita Ukonga jijini Dar es salaam  alikotembelea kuwapongeza kwa kusherehekea miaka 52 ya Jeshi la Wananchi leo Septemba
1, 2016

Rais Magufuli awataka wahandisi nchini kufanya kazi kwa weledi na uadilifu
Na Sheila Simba-MAELEZO

Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amewataka
wahandisi nchini kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kuiwezesha nchi
kufikia uchumi wa kati kupitia ujezi na uendelezaji viwanda.


Amesema hayo leo jijini Dar es salaam katika mkutano wa 14 wa Bodi ya
Wahandisi Nchini,na kuwaasa kutumia taaluma yao kusaidia nchi kufikia
uchumi wa kati ili kuleta maendeleo kwa haraka kwa watanzania.

“mkiamua
nchi iende kwenye uchumi wa kati inawezekana lakini kama mtaamua
isiendi pia inawezekana hivyo basi uzalendo unahitajika katika kufanya
kazi na kufikia malengo tuliyojiwekea,”Alisema Rais Magufuli.

Aidha
amewataka kufanya kazi kwa ushirikiano,kujitambua na kuaacha ubinafsi
miongoni mwao hasa kwenye utendaji kazi na miradi ya maendeleo.

“Tumemsikia
waziri akisema serikali inamapango wa kukarabati na kununua meli mbili,
wahandisi jiulizeni mmejipangaje kutumia fursa hii kwa kuomba tenda na
naamini serikali haiwezi kukataa ombi hasa kwa wahandisi wa
ndani”Alisema Rais Magufuli

Akimkaribisha rais Magufuli katika
mkutano huo waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa
alisema kuwa licha sekta ya miundo mbinu kufanya vizuri hasa ya ujenzi
wa barabara kwa kiwango cha lami,Serikali itaendelea kulipa kipaumbele
ujenzi wa barabara kuanzia viijiji,Halmashauri na za mikoa.

“serikali
inafanya jitahada kujenga miondo mbinu imara ili kurahisisha usafiri wa
kutoka sehemu moja kwenda nyinfine na ukarabati wa kiwanja cha ndege
cha Dodoma umekamilika kwa asilimia 98,” Alisema Prof. Mbarawa.Kwa
upande wake mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Prof.Ninatubu Lema
amemuomba Rais kutoa nafasi kwa wahandisi wa ndani kushiriki katika
miradi mikubwa ili kujifunza kupitia miradi hiyo.

Aidha Mhandisi
Lema kwa niaba ya bodi hiyo wametoa kiasi cha fedha shilingi milioni
100 kwaajili ya kusaidia katika ununuzi wa vifaa vya maabara kwa shule
za sekondari nchini.akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa mkoa wa Dar
Es Salaam Mhe.Paul Makonda alitangza tarehe mosi oktoba kuwa siku ya
kupanda miti katika mkoa wa Dae Es Salaam.

“Katika kuhakikisha
miundo mbinu inakua safi natangaza rasmi hapa tarehe mosi oktoba itakua
ni siku ya kupanda miti katika mkoa wa Dar Es Salaamu na kampeni hiyi
itaitwa MTI WANGU”alisema Makonda