Vikosi maalum vya umoja wa mataifa nchini Syria vimesema vimeridhishwa na kupungua kwa mapigano tangu usitishwaji wa mapigano kuanza siku ya jumatatu.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Staffan De Mistura amesema kuwa anatarajia usambazaji wa misaada kuanza hivi karibuni,
Amesema pia kipaumbele cha sasa ni kuandaa usambazaji wa misaada katika maeneo yaliyoshikiliwa na waasi huko Aleppo.
Mistura ameonya kuwa usitishwaji wa mapigano unaweza kuhatarishwa na athari za matukio ya vurugu yanayohusisha pande zenye mzozo.
Wizara ya mambo ya nje ya Syria imeonya kuwa vifaa havitaruhusiwa kuingia Aleppo bila ruhusa yake.
Kusitishwa kwa mapigano kumeleta utulivu katika maeneo ya wakazi yanayoshikiliwa na waasi mjini Aleppo huku watoto wakicheza nje kwa mara ya kwanza bila kuwepo kwa ndege za mashambulizi, lakini Urusi imeshutumu waasi kwa ukiukaji zaidi ya mara ishirini nchi nzima wa makubaliano ya kusitisha mapigano na kuitaka Marekani kuweka nguvu kwa kundi wanalounga mkono.
0 Comments