Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, alipofanya ziara kwenye makazi ya askari ya kigoto yalipopo Kata ya kirumba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza jana.

Wizara ya Mambo ya Ndani nchini imeahidi
kutatua changamoto mbalimbali zinazovikabili vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo
uhaba wa makazi na sale za askari ili kufanikisha vyombo hivyo kufanya kazi kwa
weledi na ufanisi mkubwa.

Waziri anayeshughulikia wizara hiyo,
Mwigulu Nchemba, ametoa agizo hilo hii leo kwenye kikao baina yake na viongozi
mbalimbali wa vikosi vya Ulinzi na Usalama mkoani Mwanza, kilichofanyika kwenye
gereza kuu la Butimba Jijini Mwanza.

Amesema jitihada za ujenzi wa nyumba
za ghorofa kwa ajili ya makazi ya askari katika miji mikuu ya Mwanza, Arusha,
Mbeya na Dar es salaam zitaenda sambamba na ujenzi wa nyumba za kawaida katika
wilaya mbalimbali nchini ili kutatua kero hiyo.

Katika hatua nyingine, Waziri Nchemba
ametoa onyo la kukamatwa wale wote wanaotoa kejeli kwenye mitandao ya kijamii
juu ya utendaji kazi wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini pamoja na askari
wanaopata madhara wakipambana na uhalifu, kama ilivyotokea katika tukio la
mauaji ya askari lililotokea hivi karibuni Jijini Dar es salaam.

Awali Kamanda wa jeshi la Polisi
mkoani Mwanza, Ahmed Msangi, amebainisha baadhi ya changamoto zinazolikabili
jeshi hilo kuwa ni pamoja na ukosefu wa makazi ya askari, uhaba wa fedha pamoja
na madeni ya askari, ambazo zikifanyiwa kazi zitaboboresha zaidi utendaji wa
jeshi hilo.

Waziri Nchemba amefanya ziara ya siku
moja mkoani Mwanza, akitokea mkoani Kagera alikoenda kujionea uhalibifu uliotokana
na tetemeko la ardhi lililotokea mwanzoni mwa mwezi huu na kuzungumza na
watendani mbalimbali wa taasisi za wizara yake, ambapo ametembelea makazi ya
askari ya Kigoto na gereza kuu la Butimba Jijini Mwanza, kabla ya kuendelea na ziara
yake hapo kesho mkoani Mara.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Kirumba Ilemela Jijini Mwanza (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba (kulia) kwenye makazi ya askari Kigoto Jijini Mwanza. Katikati ni Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi.
Maofisa mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, wakiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, kwenye makazi ya skari Kigoto Jijini Mwanza hii leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, akiwa amembeba mmoja wa watoto kwenye makazi ya askari Kigoto Jijini Mwanza.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, kushoto) akisalimiana na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, alipowasili kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.

Afisa wa polisi akitoa taarifa fupi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, kushoto) alipowasili kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahmad Msangi, akizungumza kwenye kikao baina ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, akizungumza kwenye kikao baina yake na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.

Baadhi ya Maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, wakiwa kwenye kikao baina yao na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.