Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Oct 10, 2016

Amber Lulu Afungukia Kukamatwa Na Unga

Kufuatia madai ya kukamatwa akisafirisha madawa ya kulevya ‘unga’ jijini Arusha kuelekea China, video queen matata Bongo, Lulu Auggen ‘Amber Lulu’ amefungukia ishu hiyo akidai kuwa anaamini ilitengenezwa na watu walioamua kumchafua.Amber Lulu aliliambia Wikienda kuwa alishangaa kuona mitandaoni kwamba amekamatwa na unga, lakini hakuna kitu kama hicho kwani hajawahi kukamatwa.
Kabla ya kumpata Amber Lulu, simu yake ilikuwa haipatikani hivyo Wikienda lilimtafuta mdogo wake aliyeko jijini Mbeya ambaye naye alikiri kutompata mrembo huyo hewani kwa siku tatu ambapo ndugu walimtafuta kwenye vituo vya polisi jijini Arusha bila mafanikio.
Wapo baadhi ya watu waliodai kuwa ni kiki iliyofanywa na Amber Lulu mwenyewe ili kuwafanya watu wamuongelee.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP