Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amempigia simu rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ,akimtaka kutupilia mbali uamuzi wa serikali kujiondoa katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC.
Afisi ya bwana Ban imesema kuwa inathamini jukumu la taifa hilo katika kupigania haki na kwamba inatumai taifa hilo litaangazia upya uamuzi wake.
Afrika Kusini ilisema mapema mwezi huu kwamba itajiondoa katika mahakama ya ICC kwa sababu ni kikwazo katika juhudi zake za kukuza amani barani Afrika.
Mwaka uliopita ,mahakama ya Afrika Kusini iliikosoa serikali kwa kukataa kumkamata rais wa Sudan Omar El bashir.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ban Ki-moon
Image captionKatibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ban Ki-moon

Mataifa ya Burundi na Gambia tayari yametangaza kujiondoa katika mahakama hiyo.
Siku ya Ijumaa bwana Ban aliambia baraza la usalama katika Umoja wa Mataifa kwamba alijutia mataifa yanayojiondoa katika mahakama ya ICC kwa kuwa huenda yakatoa ujumbe m'baya kuhusu jukumu lao katika kupigania haki.