Bondia maarufu nchini, Thomas Mashali amekutwa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo na mwili wake kukutwa maeneo ya Kimara, Jijini Dar es salaam. akithibitisha kutokea kwa kifo cha mwanamasumbwi huyo, Bondia Abdallah Pazi (Dullah Mbabe) amesema Mashali amefikwa na umauti huo usiku wa kumkia leo kwa kudaiwa kupigwa mpaka kuuawa na watu wasiojulikana kwa tuhuma za wizi. tutaendelea kujuzana taarifa zaidi za msiba huu wa Mwanamasumbwi huyu nguli hapa nchini,