Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwa amembeba mmoja ya mwanafunzi wa shule ya Msingi Ikungi mchanganyiko


 Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikabidhi mahitaji kwa wanafunzi walemavu mara baada ya kuwasili shule ya msingi Ikungi mchanganyiko



 Baadhiya washiriki wa Kongamano wakisikiliza kwa makini mada zikiwasilishwa kwenye mdahalo



 Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwa na baadhi ya viongozi wa ngazi ya Wilaya wakati kongamano likiendelea




 Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimsalimu Bi Fumbo Shishiwa aliyejifungua salama mtoto wa kiume na kumuita Magufuli


 Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimiana na wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya msingi Ikungi mchanganyiko


 Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akishiriki kuandaa bustani kwa ajili ya mbogamboga zitakazotumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko


Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ikungi akichangia mada iiliyokuwa inajadiliwa kwenye Kongamano la Kumuenzi Mwalimu J.K Nyerere kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ikungi

 Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimia na Bi Faidha Athumani mara baada ya kumkuta akisubiri matibabu katika Kituo cha afya Ikungi


 Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akishiriki kuandaa bustani kwa ajili ya mbogamboga zitakazotumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko


 Baadhi ya washiriki wakifatilia kwa makini Kongamano



 Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua Chumba cha kuhifadhia maiti katika Kituo cha Afya Ikungi


 Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua Mashine ya vipimo vya magonjwa mbalimbali ikiwemo ini katika kituo cha afya Ikungi


Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimuelekeza Mganga Mkuu wa kituo cha Afya Ikungi kuhakikisha anasimamia ujenzi wa upanuzi wa chumba cha kuhifadhia maiti




Na Mathias Canal, Singida


Uongozi wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida umeungana na Watanzania kote
ulimwenguni kuadhimisha kumbukizi ya miaka 17 ya kifo cha Mwasisi wa
Taifa na Rais wa Kwanza wa Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere aliyefariki dunia Octoba 14, 1999 katika Hospitali ya Mtakatifu
Thomas huko Uingereza.

Katika Kongamano hilo lililofanyika
katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ikungi limejumuisha Viongozi wa kada
tofauti wakiwemo viongozi wa serikali, Viongozi wa Dini, Viongozi wa
Vitongoji na vijiji, Viongozi wa siasa, Wazee wa mji wa Ikungi, Maafisa
Tarafa na Watendaji, Madiwani, Walimu na wanafunzi ambapo wote kwa
pamoja wamepata nafasi ya kuchangia mada na kupitisha maadhimio zaidi ya
kumi na tano yatakayotoa taswira ya namna ya kumuenzi Mwalimu Nyerere
mwakani.

Mgeni rasmi katika Kongamano hilo Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amewasihi wananchi kwa umoja wao
kumuenzi Mwalimu Nyerere katika matendo makubwa na muhimu aliyokuwa
anayafanya hususani misingi ya Haki, Ukweli na uwajibikaji.


Amewataka watanzania kuishi katika matakwa ya Mwalimu Nyerere ikiwa ni
pamoja na kutokubali kutoa na kupokea Rushwa kwani hayo ni miongoni mwa mambo
mengi aliyoyahubiri wakati akiwa waziri Mkuu kabla ya kujiuzulu nafasi
hiyo na hatimaye kuyahubiri na kuyaishi kipindi akiwa Rais wa kwanza wa
Tanzania.

Dc Mtaturu alisema kuwa Tanganyika wakati wa uhuru
ilikuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo maradhi yatokanayo na magonjwa
ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza, Pia kulikuwa na ujinga uliosababishwa na ukosefu wa elimu bora kwa kiasi
kikubwa kwani watanganyika wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu
walikuwa ni zaidi ya asilimia 90.

Alisema kuwa sambamba na hayo
pia kulikuwa na umasikini mkubwa na uliokithiri kwani asilimia kubwa ya
watanzania walikosa mahitaji ya msingi kama vile malazi, Chakula, na Mavazi
ambapo Mwalimu Nyerere alifanikiwa kupingana na maadui hao watatu kwa
kuongeza udahili kwa kiasi kikubwa katika shule muhimu za Sekondari
Kilakala, Kibaha na Mzumbe.

Mtaturu alisema kuwa pia Mwalimu
Nyerere alitaifisha taasisi zote za watu binafsi ili kuleta usawa katika
jamii pamoja na kuimarisha upatikanaji mzuri wa huduma za afya katika zahanati,
vituo vya afya, na Hospitali ili kuboresha afya za watanzania
na kuwafanya kuweza kufanya kazi vizuri na kwa ufasaha.

Dc
Mtaturu Amewataka washiri wote wa Kongamano hilo na watanzania kwa
ujumla kuendelea kuwa viungo muhimu katika kudumisha Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar, Kudumisha Lugha ya Kiswahili, Kukuza Utu na
uadilifu katika kazi na jamii inayotuzunguka.

Zaidi amesisitiza
wakulima kwa kushirikiana na maafisa kilimo kulima kilimo chenye tija
ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ili kuhakikisha wanakuwa na
mavuno mengi yenye faida kubwa na kuwaongeza uchumi wao kwani wastani wa
pato la Mtanzania aishie Wilaya ya Ikungi ni shilingi elfu mbili kwa
siku ambapo kwa mwezi ni shilingi elfu sitini.

Hata hivyo Dc
Mtaturu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa
vitendo hususani kusimamia vyema mapato ya serikali, Kupambana katika
misingi ya utu, haki na usawa kwa kila Raia wa nchi hii, Kupinga Rushwa
na matumizi mabaya ya fedha za Umma.

Kwa upande wake Kaimu Katibu
Tawala wa Wilaya ya Ikungi Ndg Dandala Mzunguor ameyataja baadhi ya
maadhimio yaliyojadiliwa katika kongamano hilo kuwa ni pamoja na Kupata
viongozi wa Haki na halali katika chaguzi zetu, Jamii kuwa na moyo wa
uzalendo na kujitolea katika kufanya kazi.

Mengine ni kuepuka
kejeli na dharau katika maisha ya kila siku, Kuboresha mazingira ya
kufundishia, Jamii na viongozi kuweka miiko ya uongozi, Kudumisha umoja
na mshikamano wa Taifa letu.

Naye katibu wa Chama Cha Mapinduzi
CCM Wilaya ya Ikungi Aluu Segamba amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kuamua kumuenzi
Mwalimu Nyerere kwa kufanya kongamano kwani imekuwa taswira njema kwa
wakazi wa Wilaya hiyo ambao hawajawahi kushiriki katika kongamano kama
hilo tangu kuanzishwa kwa Wilaya hiyo.

Baadhi ya wachangiaji
katika kongamano hilo la kumuenzi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
wamependekeza kuwa na siku moja ambayo Mkuu wa Wilaya atakutana na
wananchi wote kwa ajili ya kujadili kwa pamoja namna ya kuiboresha
Wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na shughuli za kijamii hususani kuboresha
kilimo, Uchumi na Miundombinu.

Wengine wamependekeza bendera
kupeperushwa nusu mlingoti ni kuenzi na kutoa heshima kubwa kwa Baba wa
Taifa kwani kufanya hivyo itakuwa njia sahihi ya kuongeza uwajibikaji na
nidhamu ya Taifa.

Kabla ya Kongamano hilo mkuu huyo wa Wilaya ya
Ikungi akishirikiana na viongozi wote wa Wilaya pamoja na kamati ya
ulinzi na usalama alitembelea Shule ya Msingi mchanganyiko Ikungi ili
kutoa baadhi ya mahitaji kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwemo Wenye ulemavu wa ngozi, Walemavu mchanganyiko na wasioona.


Sambamba na hayo pia amewatembelea wagonjwa katika Kituo cha afya Ikungi kwa kuzuru katika wodi za wanawake waliojifungua, sambamba na
Wodi ya wanaume na Wanawake.

Dc Mtaturu amemuagiza mganga Mkuu wa
Zahanati hiyo kuhakikisha anafanya utaratibu wa kujenga Sehemu ya
kuhifadhia maiti kutoka na sehemu iliyopo kuzidiwa kwani ina sehemu
mbili tu za kuhifadhia maiti.




Aidha Dc Mtaturu alipotembelea kituo cha Afya cha Ikungi alipitia maagizo yake aliyowahi kuyatoa hivi karibuni ya kupanua chumba cha maabara na kuagiza kutengenezwa kwa mashine ya kupimia magonjwa mbalimbali ndani ya muda mfupi ili kuboresha huduma ya afya kwa wananchi wanaotumia kituo hicho kwa ajili matibabu.

Akifunga Kongamano hilo Mkuu wa
Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amesisitiza kuwa katika
kumuenzi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni lazima kuhakikisha huduma
za Afya, Elimu, Uchumi, Kilimo na Miundombinu zinaboreshwa.