Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alipotembelea wodi ya wanawake

Watumishi, wauguzi na madaktari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alipozuri katika hospitali ya Manispaa ya Ubungo kwa ziara ya kikazi


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwasili Ofisi za Manispaa ya Ubungo


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Akitoa maelekezo wakati akikagua ufanisi wa kazi katika Hospitali ya Manispaa ya Ubungo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisikiliza kwa makini maelezo ya jinsi wanawake wanavyohudumiwa katika wodi ya wanawake


Na Mathias Canal, Dar es salaam



Duka la Dawa za Binadamu lililopo katika Hospitali ya Manispaa ya
Ubungo iliyopo katika Mtaa wa Sinza Jijini Dar es salaam limekutikana na
unadhilifu wa fedha za Umma kinyume na utaratibu wa matumizi ya fedha
hizo.



Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
ameyabaini hayo baada ya kukagua mapato na matumizi ya Duka hilo na
kugundua uwapo wa ubadhilifu huo mdogo mdogo ambao ameahidi kutuma
mkaguzi wa ndani ili kukagua hesabu za duka hilo.



MD Kayombo
amebainisha hayo wakati wa kikao cha kazi na watumishi wa Hospitali hiyo
mara baada ya kuzuru na kuwa na kikao cha pamoja ili kukumbushana
majukumu ya kazi ikiwa ni pamoja na kujitambulisha ili kisikiliza kero
za watumishi hao na kuzitafutia ufumbuzi.



Kayombo amebaini kuwa
Duka hilo la Dawa za binadamu katika Hospitali ya Manispaa ya Ubungo
lina Account mbili zilizofunguliwa kwa ajili ya matunzo ya fedha za
mauzo jambo ambalo sio sahihi kisheria katika Taasisi moja ya serikali
kuwa na Account mbili za Bank.



MD Kayombo ameahidi kubadilisha
Mfumo wa kukusanya Mapato katika Hospitali hiyo kuhamia mfumo wa kisasa
ili Serikali iweze kukusanya fedha za kutosha ambapo mfumo wa sasa
mapato mengi yanapotea kwani kufanya hivyo itarahisisha Hospitali hiyo
kuweza kujisimamia katika maswala ya matumizi madogo madogo na kuweza
kuongeza uwezo wa kunua dawa za kutosha kwa mahitaji husika.



Kuhusu kutoa na kupokea Rushwa MD Kayombo amesema kuwa hakuna
asiyetambua kuwa jambo hili linawanyima haki wananchi wengi wanyonge
hivyo watumishi wote katika Hospitali hiyo wameonywa kujihusisha na
kadhia hiyo kwani endapo mtumishi yeyote atabainika kufanya hivyo
atachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo ili kuwa fundisho kwa wengine.



"Watumishi wote mnatakiwa kuwa Clean Officials katika mazingira ya kazi
hivyo ni lazima kujiepusha na ubadhilifu wa fedha za Umma kwani kila
mmoja anapaswa kuridhika na kipato anachopata, Pia nawaahidi kila mmoja
kumpatia Extra Duty Allowance kulingana na Bajeti ya mwaka wa fedha
2016/2017.



MD Kayombo ametembelea Wodi zote Hospitalini hapo na
kujionea hali halisi ya utoaji huduma ambapo pia ametembelea Ofisi zote
zinazotoa huduma na kukutana na wataalamu mbalimbali ambapo wameelezea
changamoto zao jambo ambalo Mkurugenzi huyo ameahidi kulifanyia kazi
haraka iwezekanavyo kwani lipo ndani ya uwezo wake.



Md Kayombo
Amewaonya Wakuu wa Idara kuacha tabia ya kuwanyanyasa na kuwagawa
watumishi katika sehemu za kazi ili kuongeza ufanisi katika utendaji
kazi katika kuwahudumia wananchi.



Kwa upande wao baadhi ya
watumishi katika Hospitali hiyo wamempongeza Mkurugenzi huyo wa Manispaa
ya Ubungo kwa ziara yake katika Hospitali hiyo kwani amekuwa Mkurugenzi
wa kwanza kuzuru Hospitalini hapo na kujionea hali halisi ya utoaji
huduma na sio kusimuliwa.



MD Kayombo ametoa namba ya simu kwa
ajili ya matumizi ya dharura kwa watumishi hao ili waweze kuripoti
matukio ya haraka ambayo yanakuwa nje ya uwezo wao.