Leo Oktoba 19{jana}, 2016 Kamati ya Shindano la Maandalizi ya Miss Tanzania 2016 imesema Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika Oktoba 29,10, 2016 katika viunga vya Rock City Jijini Mwanza, litakuwa bora zaidi kutokana na maandalizi yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika.

Na BMG
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hashim Lundenga (kulia) ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Rhino Agency inayoandaa Miss Tanzania, amesema baada ya mashindano hayo kufanyika Jijini Dar es salaam miaka yote, kamati hiyo imeamua yafanyike Jijini Mwanza na kwamba yatafanyika kwa miaka mitano mfululizo.

Amesema washiriki wote 30 katika shindano hilo ni bora hivyo yeyote atakayeibuka mshindi ataliwakilisha vyema taifa kwenye mashindano ya Miss World yanayotarajiwa kufanyika Disemba 18, 2016 Jijini Washingtone DC nchini Marekani.

Viingilio katika shindano hilo ni shilingi 20,000, 50,000 na 100,000 ambapo inategemewa kwamba wasanii Ali Kiba pamoja na Christian Bella ikiwa wataafiki makubaliano watadondosha burudani katika shindano hilo huku washiriki wakijipatia fursa mbalimbali ikiwemo mshindi wa kwanza kujishindia gari.

Washiriki wa shindano hilo wamesema wamejiandaa vyema na bado wanaendelea kujinoa zaidi ili kuhakikisha atakayeibuka mshindi anaiwakilisha vyema Tanzania kwenye mashindano ya dunia huku wakielezea furaha yao kubwa kwa mashindano hayo kufanyika Jijini Mwanza kwa mara ya kwanza.
Kamati ya Miss Tanzania 2016 ambapo kutoka kulia ni Hashim Lundenga, Pamela Irengo, Flora Lauwo.
Mkutano baina ya Kamati ya Miss Tanzania 2016 na Wanahabari Jijini Mwanza
Washiriki wa Miss Tanzania 2016 katika ubora wao