Hawa ndio baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma katika shule ya sekondari ya Malangali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya  kuwasili katika shule hiyo na kukaangalia mazingira ya shule hiyo na kutafuta njia za kutatua baadhi ya changamoto kwa kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania
mkurugenzi wa kampuni ya Yono action mart Yono Kevela ambaye ni mlezi wa kundi la Malangali Alumni association (MAAS) akizungumza mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari Malangali na kuwaeleza jinsi gani shule hiyo ilivyowapo mafanikio hadi sasa walipofikia.




 na fredy mgunda,Iringa


Wanafunzi waliowahi kusoma
shule ya sekondari ya Malangali iliyopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
wamewataka vingozi,wafanyabiashara,wakulima na wajasiliamali mbalimbali walinufaika
na elimu kutoka shule ya malangali kurudisha fadhila katika shule hiyo.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi
wa kampuni ya Yono action mart Yono Kevela ambaye ni mlezi wa kundi la
Malangali Alumni association (MAAS) alisema kuwa maendeleo aliyoyapata sasa ni kutoka
na shule ya mangali hivyo ameamua kurudi na kuisadia shule hiyo. 

“Wafanyakazi na viongozi
mblimbali tunatakiwa kuboresha mazingira na miundombinu ya shule tulizosoma ili
kuendeleza na kukuza elimu ya hapa nchini tanzania.” Alisema Kevela

Kevela amesema kuwa shule
nyingi walizosoma viongozi,wafanyabiasha na wajasiliamali mbalimbli
zinahitajika kukarabatiwa hivyo amewataka wadau wote kuzikumbuka shule
walizosoma.

Naye Padre wa kanisa la
kikatoriki mkoani mbeya Telesipholi Tweve aliwakata wanafunzi mbalimbali
waliosoma katika shule kongwe kurudisha upendo katika shule hizo kwa kuwa ndio
chanzo cha mafanikio yao ya leo.

“Leo nimerudi katika shule
hii ya malangali kuja kusaidia kutatua changamoto ambazo zipo katika shule hii
ukizingatia kuwa shule hii inauchakavu wa majengo na miundombinu hivyo sisi
kama MAAS tumeanza kwa kukarabati ukumbi ambao utakuwa na faida kwao kwa
kutumia kwenye sherehe na kukodishwa pia”.alisema Tweve

Kwa upande wake mwenyekiti
wa Malangali Alumni association (MAAS) Paul Mng’ong’o alisema kuwa wameanza
kuisaidia shule ya Malangali muda mrefu kwa kuwa tayari wameshakarabati ukumbi
wa shule,wamewanunulia tv na king’amuzi kwa ajili ya habari na wanaendelea
kutatua matatizo ya shule hiyo.

“Hebu angalia sisi tuliosoma
hapa tumepata mafanikio lakini shule yetu bado ipo pale pale na inazidi
kuchakaa hivyo inatulazimu kuchangishana ili kurudisha fadhila kwa kuwa wengi
wetu tumepata mafanikio makubwa kutoka shule hii,tunaviongozi wengi,matajili
wengi ,wakulima wakubwa sana hapa nchini wote wamesoma katika shule
hii”.Alisema Mng’ong’o

Lakini pia Mng’ong’o alisema
kuwa lengo la kundi la Malangali Alumni Association kuunganisha wanafunzi wote
waliowahi kusoma shule ya secondary ya Malangali na kuweza kupeana malengo na
kusaidiana pale wanapokwama kimalengo.



Shule ya Malangali ni kati ya shule kongwe ambazo viongozi mbalimbali katika serikali,taasisiza Umma na sekta walijengewa msingi wa kwanza wa maisha.


kaika mwaka wa bajeti huu serikali imetenga bajeti ya kukarabati shule kongwe zipatazo thelethini na saba (37) jambo ambalo wananfunzi hao wameomba serikali kuharakisha utekelezaji wake.