Unyanyasaji kingono na hata pia ghasia dhidi ya wabunge wanawake umeongezeka, ripoti mpya ya kundi la wabunge duniani inasema.
Utafiti huo wa Muungano wa mabunge (IPU) inachapishwa katika mkutano wa kila mwaka wa kundi hilo Geneva.
Wabunge 55 wanawake pekee ndio walioshiriki katika uchunguzi huo, lakini wanawawakilisha wabunge kutoka kote duniani.
Zaidi ya asilimia 80 wamesema wamepitia aina fulani ya unyanyasaji wa kiakili au kingono au hata pia ghasia.
Tisho la kubakwa
Ripoti hiyo ya IPU inajiri wakati matamshi ya mgombea urais Marekani Donald Trump dhidi ya mpinzani wake, Hillary Clinton, na tuhuma dhidi yake za unyanyasaji wa kingono wa wanawake wengine katika miaka ya nyuma, yamegubika vyombo vya habari.
Inafichua baadhi ya visa vya unyanyasaji vinavyowakabili wabunge wanawake duniani wakiendelea na majukumu yao katika nyadhifa walizochaguliwa.
Mbunge wa bunge la Ulaya amearifu kuwa amepokea vitisho zaidi ya 500 vya kubakwa katika mtandao wa Twitter katika muda wa siku nne tu.
Mwingine kutoka Asia, alipokea vitisho vya mwanawe wa kiume kutendewa vibaya, vilivyo eleza shule anakosoma, darasa lake na hata umri wake.
Kati ya wanawake walioshiriki katika utaifiti huo, 65.5% wamesema wamelengwa kwa matusi machafu. Ripoti hiyo imeashiria kuwa ni kawaida kwa wafanyakazi wenza wanaume kuwatolewa matamshi machafu.
"Katika sehemu ninayoishi… kuna kila aina ya lugha inayolinganisha wabunge wanawake," anasema Prof Nkandu Luo, ambaye sasa ni mbunge wa jinsia Zambia.
Anakumbuka mbunge mwenzake mwanamume akieleza hadharani kwamba anapenda kwenda bungeni kwasababu "wanawake wote wako huko na anaweza kunyoosha kidole na akachagua anayemtaka".
Matamshi hayo yaliripotiwa kwenye vyombo vya habari kama jambo linalofurahisha na linalokubakila. "Ndivyo namna wanavyo dharau wanawake."
Unyanyasaji kingono
Wakati huo huo, Senata Salma Ataullahjan wa Canada amesema mara ya kwanza alidhani utafiti huo hauna maana kwake.
Lakini amesema amehamasika katika kujibu maswali ya utaifiti huo. "Unajua sisi kama wabunge, tunakwenda nje tunakutana na watu na namkumbuka huyu mwanamume mmoja aliyenikaribia sana."
Alianza kutoa matamshi yasio na heshima kwa Sen Ataullahjan, ambayo kwa wakati huo aliya puuzilia mbali.
Lakin kwa kuzngumzia tukio hilo katika utafiti huo ilimzindua kwamba alikabiliwa na tabia isiyo sawa, na ya kutishia.
Sasa anasema amekuwa wazi zaidi na wafayanyakazi wenzake wa kiume.
"Ni lazima tubadili fikra zetu kuhusu lugha na tabia inayokubalika na isiyokubalika," anasema.
Ripoti hiyo inamaliza kwa kueleza kuwa unyanyasaji wa kingono , matamshi ya matusi na kuaibisha na hata pia ghasia zinawazuia wanawake wengi waliochaguliwa kutekeleza majukumu yao kwa uhuru na kwa salama.
0 Comments