katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani Iringa  kwaridela vijana wa cahama cha mapinduzi wilayani Mufindi wakati wa sherehe siku ya vijana wa chama cha mapinduzi
 mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi Yohannis Kaguo kushoto akiteta jambo na katibu mkuu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa Hassani Mtenga wakati kukagua mabanda ya maonyesho yaliyofanyika katika  ofisi za CCm wilaya ya Mufindi


katibu wa
UVCCM Mufindi Fatuma Ngailo na

mwenyekiti wa vijana wa chama cha mapinduzi
wilayani Mufindi felix Lwimbo wakielekea kufanya usafi katika hospitali ya mafinga


hawa ni baadhi ya vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Mufindi wakiwa wamemaliza kufanya usafi katika hospital ya mji wa Mafinga wakiongozwa na katibu msaidizi wa mufindi.



na fredy mgunda,iringa


VIJANA wa chama cha
mapinduzi (CCM)wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa wamewataka wafanyakazi na
viongozi wa serikali kufanya kazi kwa kujituma ili kumuenzi mwalimu Nyerere kwa
vitendo.

Haya yalisemwa na katibu wa
UVCCM Mufindi Fatuma Ngailo wakati akisoma lisala kwa mgeni rasmi wakati wa
maazimisho ya siku ya vijana wa chama cha mapinduzi yaliyofanyika wilayani
Mufindi.

viongozi wa vyama vya Siasa
wametakiwa kuiga kwa vitendo uzalendo na moyo wa kujitoa  aliokuwa nao Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere enzi za uhai wake  ili
kuliwezesha Taifa kupiga hatua kimaendeleo.

“nitahakikisha nazilinda
mali za taifa,nasisitiza uwajibika,uzalendo,uandilifu na nidhamu katika
kulitumikia taifa la Tanzania kama unakumbuka mwalimu alikuwa anapenda kutumia
neno (it can be done play your part) kila mtu atimizi majukumu yake” Alisema Ngailo

Amesema kuwa kumbukumbu za
Baba wa Taifa zilizohifadhiwa vizuri katika makumbusho hiyo zina mambo mengi ya
kujifunza ambayo wanasiasa wanatakiwa kuyafanya kwa  vitendo hasa
uzalendo kwa nchi, uvumilivu, upendo
na moyo wa kujitoa kwa dhati kuwatumikia wananchi.

“Kupitia kumbukumbu hizi
sisi vijana tumejifunza ukomavu wa demokrasia aliokuwa nao Mwalimu Nyerere
akiwa ndani na nje ya Bara la Afrika,wengi wanadhani Demokrasia ni wakati wa
uchaguzi tu, kumbe demokrasia ni pamoja na kuheshimu watu wengine” Alisema Ngailo

Akiongea kwenye sherehe hizo mwenyekiti wa vijana wa chama cha mapinduzi
wilayani Mufindi felix Lwimbo Alieleza kuwa maisha aliyoishi Baba wa Taifa ni
mfano wa kuigwa na viongozi na watanzania wote hasa pale alipojitofautisha na
viongozi wengi wa Bara la Afrika alipoepuka tamaa ya madaraka na mali kwa  manufaa ya taifa.

“Sote ni mashahidi kupitia
kumbukumbu zake tumeona mahali alipokuwa anaishi mwalimu kabla hajajengewa
nyumba na Jeshi  kama Rais mstaafu wengi
walitegemea asingeishi katika  eneo lile,
kumbukumbu hii nzuri aliyoiacha inatufundisha watanzania kuwa mwalimu
aliitanguliza Tanzania mbele kuliko maslahi yake binafsi” Amesisitiza Lwimbo


Lwimbo amebainisha kuwa  serikali itaendelea  kumuemzi Baba wa Taifa kwa yale aliyoyafanya
na kuyasimamia kwa manufaa ya taifa huku akitoa wito kwa  viongozi wa vyama vya Siasa wawe na kiasi na
waridhike na vile walivyonavyo.

“Suala la kuridhika na kuwa
na kiasi linapaswa kuzingatiwa, wanasiasa wanapaswa kuwaheshimu wananchi
wanaowachagua kupitia chaguzi mbalimbali,
matokeo yanapotoka kama ni sahihi basi wanasiasa wakubaliane na maamuzi
yao”  Ameainisha Lwimbo

Lwimbo amemalizia kwa
kuwataka watendaji wote wa serikali ya wilaya ya Ileje kufanya kazi kwa
uaminifu,uadilifu,kuwajibika kwenye majukumu yao na kujituma na kamwe hata kuwa
tayari kuwavumilia watendaji ambao ni wazembe kazini.

Kwa upande wake katibu wa
CCM mkoani Iringa Hassani Mtenga ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi katika sherhe
hizo alisema kuwa watanzania wanayo mengi ya kujifunza kupitia vitu
alivyoviacha Baba wa Taifa ambavyo vimehifadhiwa katika Makumbusho hiyo.



Amesema kuwa maisha ya
uadilifu aliyoishi enzi za uhai wake na mchango wake katika kuiletea maendeleo
Tanzania na Bara la Afrika vinapaswa kuenziwa kwa nguvu zote na viongozi wa
Tanzania.

“kwa wale mliopata nafasi ya
kuitembelea makumbusho na jua mmejifunza vitu vingi kumhusu Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere kwamba alikuwa ni mtu wa namna gani kwa viwango vya Afrika na
dunia kutokana na kumbukumbu ya uadilifu aliyoiacha ndani na nje ya mipaka ya
Tanzania” alisema Mtenga

Naye mwenyekiti wa CCM
wilaya ya Mufindi Yohannes Kaguo aliwataka vijana kuacha kulalamika kwa kukosa
ajira kutoka na mfumo wa serikali na kuwaomba wajitume na kuwa wabunifu ili
waweze kujiajiri wenyewe.

“Saizi unakuta vijana wengi
wanashinda mitaani na kupiga siasa tu na sio kupanga mipango ya kutatua
changamoto zao za kimaendeleo ,saa moja asubuhi unawakuta vijana kwenye mabao,pooltable
na draft sasa unafikiri hapo utapata maendeleo”alisema Kaguo