Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Nov 2, 2016

Baiskeli kulipia kuegesha Bujumbura

Waendeshaji baiskeli, Pikipiki na magari katika mji mkuu wa Burundi Bujumbura wataanza kulipa ada ya kuegesha. Serikali inanuia kukusanya mapato zaidi baada ya wafadhili wa magharibi kukata msaada wake kwa nchi hiyo.
Nchi za magharibi zinazofadhili Burundi zilighathabishwa na hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania Urais kwa muhula wa tatu, pamoja na kutumia nguvu kuzima maandamano.
Serikali pia imefuta ufadhili wake kwa Vyuo Vikuu na badala yake wanafunzi wote watagharamia ada za masomo punde wakiajiriwa baada ya kufuzu.Ada mpya za kuegesha katika jiji kuu ni dola mbili kwa baisikeli na dola 60 kwa malori makubwa.
Mabasi ya uchukuzi wa umma yatalipa dola sita kwa mwezi. raia wengi wanahofia ada mpya huenda zikasababisha mfumuko wa bei ya bidhaa. Wakaazi wengi katika mji mkuu tayari wanalalamikia ongezeko la gharama ya maisha na wafanyikazi wengi hupokea dola 80 kwa mwezi.

Raia waliandamana kupinga hatua ya Rais kuwania mhula wa tatuImage copyrightREUTERS
Image captionMamlaka zimetumia nguvu kuzima maandamano

Muungano wa Ulaya ulisimamisha msaada kwa serikali ya Burundi na kusema Mamlaka hazijasaidia kurejesha utulivu nchini.Msaada wa Muungano wa ulaya kwa Burundi ulikadiriwa kuwa dola milioni 470 kati ya mwaka 2014 hadi mwaka 2020.
Zaidi ya watu 400 wameuawa na wengine laki mbili unusu kukimbilia katika nchi jirani kufuatia machafuko ya kisiasa yaliyozuka baada ya Rais Nkurunziza kuamua kuwania mhula wa tatu.
Mwezi uliopita Burundi ilitangaza kujiondoa kutoka uwanachama wa mahakama ya kimataifa ya jinai ICC.Tangazo hili lilitolewa miezi sita baada ya mwendesha mashtaka mkuu wa ICC kusema atachunguza ghasia nchini humo.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP