Mkurugenzi wa FBI, James Comey ameliambia bunge la Marekani kuwa baada ya kupitia barua pepe zilizogundulika kutoka kwa Hillary Clinton, wakati alipokua waziri wa mambo ya nje wamegundua kuwa hana hatia yoyote na hawatamfungulia mashtaka.
Kampeni za Clinton ziliingia doa wiki iliyopita baada ya mkurugenzi huyo wa FBI kusema kuwa watazipitia barua pepe zake zilizopatikana katika kompyuta ya msidizi wa zamani wa mume wake.
Kauli hiyo imeonekana kumfurahisha mkuu wa mawasiliano wa kampeni za Clinton Jennifer Palmieri.

Marekani
Image captionDonald Trump,mgombea urais nchini Marekani

Wakati upande wa Bi Clinton wakifurahia hatua hiyo kwa upande wake Donald Trump amesema Hillary Clinton analindwa na mfumo wa wizi wa kura, amesema Bi Clinton angetakiwa kuchunguzwa kwa muda mrefu.
Na hivi sasa tunaunana moja kwa moja na Zuhura ebu tuambie baada ya FBI kusema hawatamshtaki Hilary Clinton, hali ikoje kwa sasa ikiwa ndio imebaki takribani siku moja uchaguzi ufanyike.