Fidel Castro, kiongozi wa zamani wa Cuba aliyeongoza mapinduzi ya Kikomunisti, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90, kakake ametangaza.
Fedel Castro aliyekuwa kiongozi wa mapinduzi ya Cuba alifariki saa nne na nusu za usiku kwa saa za Cuba.
Chini ya uongozi wa Fidel Castro, Cuba ilikuwa na uhusiano maalum na Afrika.
Katika miaka ya 1970 na 80, maelfu ya madaktari na walimu walikwenda Afrika na idadi sawa ya askari wa Cuba walipelekwa huko kuingilia kati migogoro na wakala wa vita baridi hasa nchini Angola.