Rais wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Joseph Kabila, amewahakikishia raia wake kwamba ataheshimu katiba ya nchi na kwamba hatawania urais katika Uchaguzi mkuu ujao.
Akilihutubia bunge la taifa, Kabila ameomba kuwepo amani na utulivu.

"Kwa wale ambao wanaingilia kati maisha yangu ya siasa kila siku, nina sema asante lakini wafahamu ya kwamba Jahmuri ya Kidemorisia ya Congo ni nchi inayoongozwa na katiba hatujakiuka katiba na tutaendelea kuiheshimu. Kwa mda huu kilicho muhimu ni kuangalia maisha ya wakongomani" Alisema Kabila.
Jana waziri mkuu Augustina Matata Ponyoa alijiuzulu kutoa nafasi wadhifa huo kuchukuliwa na upinzani kwenye utawala wa mpito.
Hatua hii ni ya kutuliza msukosuko wa kisiasa nchini DRC baada ya vyama vikuu vya kisiasa kususia mazungumzo ya kitaifa.