Meya mmoja nchini Ufilipino ambaye alizuiliwa kwa kushiriki kwenye ulanguzi wa madawa ya kulevya ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa korokoroni.
Polisi wanasema kuwa Rolando Espinosa ambaye ni meya wa mji wa Albuera aliuawa akiwa na mfungwa mwenzake baada ya kuwafyatulia polisi risasi walipokuwa wakifanya msako kutafuta silaha haramu.
Bwana Espinosa ni mmoja wa maafisa zaidi ya 150 waliotajwa mwezi Agosti na rais Rodrigo Duterte, kama sehemu ya kampeni ya kuwaweka hadharani wale wanaoshiriki biashara ya madawa ya kulevya. Alikuwa amejisalimisha akidai kuwa alihofia maisha yake

Sera za Rais Duterte za kupambana na madawa ya kulevya zimepigwa vikaliImage copyrightEPA
Image captionSera za Rais Duterte za kupambana na madawa ya kulevya zimepigwa vikali

Wiki iliyopita meya mwingine ambaye alitajwa na Duterte aliuawa wakati wa ufyatuliaji wa risasi na polisi kusini mwa ufilipino.