Dkt.Leonald Subi

Na George Binagi-GB Pazzo
Mganga Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonald Subi, amewahimiza wananchi kuwa na desturi ya
kupima afya zao mara kwa mara hususani kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ili
kuepukana na madhara yake ikiwemo vifo vinavyofikia asilimia 27 nchini.


Dkt Subi aliyasema
hao wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bure ya uchunguzi wa saratani ya matiti na
mlango wa kizazi mkoani Mwanza, inayofanyika kwa siku mbili kuanzia jana katika
Uwanja wa Furahisha, Vituo vya afya Igoma, Karumbe na Makongoro.

Aidha
Dkt.Subi aliwahimiza wanajamii kubadili mfumo wa maisha kwa kuzingatia kanuni
za afya ili kuepukana na madhara yatokanayo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza
ambayo ni pamona na kansa, presha pamoja na kisukari.

“Magonjwa
haya yanatokana na namna ya maisha tunavyoishi ikiwemo kutokufanya mazoezi,
ulaji wa chakula usiozingazi kanuni, ulevi, uvutaji wa sigara, kuwa na wapenzi
wengi na kutokuzingatia kanuni za afya kwa ujumla”. Alisema Dkt.Subi.

Kampeni ya
uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi inaratibiwa na Chama cha
Madaktari Wanawake nchini MEWATA katika mikoa ya Mwanza, Iringa na Mbeya kwa
lengo la kuhamasisha wananchi kupata huduma mapema kwani magonjwa yasiyo ya
kuambukiza ikiwemo saratani hutibika ikiwa mgonjwa ataanza matibabu mapema.
Tazama HAPA Picha za Uzinduzi