Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Nov 19, 2016

Mhamiaji ajiwasha moto ndani ya benki Australia

Mwanamume aliyejiwasha moto ndani ya Benki moja mjini Melbourne, Australia hapo jana ametambuliwa.
Yasemekana mtu huyo anatokea Myanmar na amekuwa akitafuta hifadhi nchini Australia. Habari zaidi zinasema aliwasili nchini humo miaka mitatu iliyopita.
Mtu huyo mwenye umri wa miaka 21 alipelekwa hospitali kupata matibabu chini ya ulinzi wa maafisa wa usalama baada ya tukio hilo.

Watu watano walipata majeraha ya moto na 21 kuathiriwa na moshiImage copyrightEPA
Image captionWatu watano walipata majeraha ya moto na 21 kuathiriwa na moshi

Wanachama wa jamii ya waislamu wa Rohingya mjini Melbourne wamesema mtu huyo aliogopa kurudi Myanmar na kwamba alikuwa anakabiliwa na changamoto za kimaisha.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP