Mke wa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema aitwaye Neema Tarimo amefikishwa mahakamani mkoani Arusha kwa kosa la kumtusi Mkuu wa Mkoa huo, Mrisho Gambo.
Neema amefikiswa mahakamani hapo na kusomewa shtaka la kumtukana mkuu wa mkoa kwa kumtumia ujumbe mfupi wa simu (sms) kupitia simu yake wenye neno ‘shoga’.

Mke wa mbunge huyo amekana kumtusi Mhe. Gambo akidai kuwa neno shoga siyo tusi bali ni neno ambalo hulitumia kuwaita marafiki zake.
“Ni kweli leo nimefikishwa mahakamani kwa shtaka la kwamba namba yangu imetumika kumtumia meseji ya matusi Mkuu wa Mkoa wa Arusha kupitia simu yangu ya mkononi lakini siyo kweli, sijamtumia meseji ya matusi na meseji niliyosomewa siyo ya matusi kumuita mtu ‘shoga’ ni kitu cha kawaida mimi nina mashoga wengi hivyo kumuita mtu ‘shoga’ sielewi kwa nini amechukulia hivyo.
Simu iliyotumika kweli ni yangu ila mahakama itaamua iwapo ni tusi au siyo tusi ila mimi na mkuu wa mkoa tunawasiliana hata katika namba yangu nyingine ninayotumia tulishawi kuwasiliana kwa meseji za kawaida au kupitia Whatsapp”. Alisema Neema
Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Augustino Rwezire ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 15 na Neema aameachiwa kwa dhamana.
Tupia Comment Yako Hapa