Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamood Mgimwa na katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani iringa Hassan Mtenga wakifuatila mchezo wa fainali katika kata ya Ikwea ambapo mshindi alipata ng'ombe mmoja na mshindi wa pili akipokea zawdi ya mbuzi mmoja ambapo zawadi zote hizo zimetolewa na mbunge huyo.
katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani iringa Hassan Mtenga akikabidhi ng'ombe kwa mshindi wa kwanza katika kata ya Ikwea ambapo mshindi wa kwanza ilikuwa timu ya Ugenza
FC walipata Ng’ombe mkubwa na mpira mmoja.

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamood Mgimwa na katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani iringa Hassan Mtenga walipomkabidhi zawadi  mshindi wa pili Ikwea
FC mbuzi mmoja na mpira mmoja

na fredy mgunda,mafinga




MASHINDANO ya Mpira wa miguu
yaliyodhaminiwa na Mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa
yanayojulikana kama Mgimwa Cup yamefika tamati katika tarafa ya Sadan yenye
kata tatu ambazo Ikwea,Sadan na Igombavanu na fainali zote zilifanyika katika
kata husika ambapo kila mshindi wa kata alipata ng’ombe mmoja na mshindi wa
pili alipata mbuzi moja,hivyo jumla ya ng’ombe tatu na mbuzi tatu zimetolewa
katika tarafa ya Sada.
Katika fainali ya kwanza
ilichezwa katika viwanja vya kijiji cha Ugenza iliyopo katika kata ya Ikwea
ilishuhudiwa timu ya Ugenza FC wakiibamiza timu ya Ikwea FC kwa goli 1-0 katika
mchezo wa vuta nikuvute.

Baada ya mchezo huo katibu
wa chama cha mapinduzi  mkoa wa Iringa
Hassani Mtenga alikabidhi zawadi mbalimbali kwa washiriki wa michuano hiyo
ambapo m
shindi wa tatu ambaye
ilikuwa timu ya Victoria FC alizawadiwa mipira miwili, mshindi wa pili Ikwea FC
walipata mbuzi mmoja na mpira mmoja na mshindi wa kwanza ambaye ni Ugenza
FC walipata Ng’ombe mkubwa na mpira mmoja.

Mtenga aliwaasa wachezaji
kuithamini michezo kwa kuwa sasa ni ajira hivyo wanajukumu la kujituma na kuipa
kipaumbe michezo na kuacha tabia za kukaa kwenye vijiwe na vilabu ambako
wanapoteza muda kwa kujadili mambo yasiyo ya msingi.

Akifunga mashindano hayo mbunge
wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa aliwaomba vijana hao wajiunge
katika vikundi ili waweze kupata fedha kwa ajili ya kuanzisha miradi ya maendeleo
ambapo itawasaidia kukuza uchumi wao na wa Taifa.

"Mimi kama Mbunge
ambaye nimetokea katika kata hii nimevutiwa sana na ninaguswa na matatizo
yanayowakabili vijana hasa katika ajira na michezo hii imefungua ukurasa mpya
kwenu nawaomba vijana wote mjiunge katika vikundi ili tuweze kuwasaidia kwa
kuwapatia fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali,"alisema makilagi.

Mgimwa alisema kuwa ligi
hiyo itakuwa ikichezwa kila mwaka huku shughuli za maendeleo kwa vijana hao
zikiendelea kama alivyowaahidi kuwa atawatafutia fedha kwa ajili ya maombi yao waliyotoa
kwa mbunge huyo.

Naye mgeni rasmi katika
fainali ya kata ya Sadan Yohanies Kaguo ambaye ni mwenyekiti wa chama cha
mapinduzi (CCM) alishuhudia timu ya Kibada fc ikiibuka mshindi kwa kuifunga
timu ya Ihanzutwa fc goli moja kwa bila na kuwakabidhi washindi ng’ombe mmoja na
mshindi wa pili alikabidhiwa mbuzi mmoja.

Kaguo aliwataka wachezaji wa
timu zote za kata ya Sadan kutunza vipaji vyao kwa kuwa ndio ajira yao na kuongeza
kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais DR John Pombe Magufuli wamedhamili
kuvithamini vipaji vyote nchini na kuvigeuza kuwa ajira kwao.

“Angalia wakina Thomas
Ulimwengu,Mbwana Samatta na wachezaji wengi wanavyonufaika na vipaji vyao vya
michezo hivyo na nyinyi mnatakiwa kujituma ili kufikia mafanikio waliofika
baadhi ya hao wachezaji” alisema kaguo.

Kwa upande wa kata ya
Igombavanu mgeni rasmi alikuwa katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi
(CCM) Jimson Mhagama naye alishudia timu ya Lugoda fc ikiibuka mshindi na
aliikabidhi timu hiyo zawadi ya ng’ombe mmoja na mshindi wa pili alipewa mbuzi
mmoja.

Mhagama alimpongeza mbunge
wa jimbo la Mufindi Mahamood mgimwa kwa jitihada za kuinua na kuibua vipaji
vipya kutoka kwenye jimbo lake.

"Kutoa ng’ombe mmoja na mbuzi
mmoja kila kata sio jambo dogo linahitaji kujipanga sana hivyo mnapoona
mashindano kama haya mnapaswa kuyakimbilia na kushiriki kikamili ili kuibuka
washindi na kuweka historia kwa kuwa mabingwa" alisema mhagama


Mashindano ya Mgimwa cup
yatafanyika katika tarafa zote za jimbo la Mufindi kaskazi na jumla ya ng’ombe
kumi na moja na mbuzi kumi na moja zitatolewa kwenye jimbo la Mufindi
kaskazini.