Mkali wa wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz aliyetamba na kibao chake cha “Baadae” ametuletea burudani mpya akiwa na Alikiba inaitwa ‘Kajiandae’ ambayo imefanywa na muongozaji mwenye kipaji kutoka Afrika Kusini, Justin Campus wa Gorilla Films ambayo unaweza kuipakua kutoka Mkito kwa kubofya hapa http://bit.ly/Kajiandae

Hii inakuwa kolabo ya pili kati ya Ommy Dimpoz na Alikiba baada ya miaka minne. Alikiba yuko chini ya usimamizi wa Studio ya Kimataifa ya ROCKSTAR4000 na Rockstar Publishing wakati Ommy Dimpoz yuko chini ya PKP Management.
 
Wimbo huu uliobeba ujumbe wa mapenzi unazungumzia mwanamke wa ndoto zao uliandikwa na Ommy Dimpoz pamoja na Alikiba na kufanyiwa kazi na mtayarishaji Emmma The Boy. Video pia iko tayari katika chaneli ya YouTube ya AliKiba na unaweza kuitizama hapo chini. Pakua : http://bit.ly/Kajiandae kisha tupe mrejesho wako