Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Nov 16, 2016

Rais Magufuli akutana na Thabo Mbeki

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Mhe. Thabo Mbeki ambapo viongozi hao wawili wamezungumzia masuala mbalimbali kuhusu Umoja wa Afrika (AU).

Pamoja na kuzungumzia masuala yahusuyo Umoja wa Afrika, Rais Mstaafu Thabo Mbeki amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Mstaafu Thabo Mbeki pia amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa alizozifanya katika uongozi wa nchi kwa kipindi cha mwaka mmoja aliomo madarakani.
Kwa upande wake Rais Magufuli amemshukuru Rais Mstaafu Thabo Mbeki kwa kumtembelea na kufanya nae mazungumzo na pia amempongeza kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Usomi na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP