Rais mteule wa Marekani Donald Trump aliyefanya kampeini ya kupinga Bima ya afya inayofaahamika kama Obama care, sasa amesema atafanyia marekebisho machache kipengee cha sheria juu ya bima hiyo ya matibabu kwa gharama nafuu.

Katika mahojiano ya kwanza tangu achaguliwe rais siku ya Jumanne, Trump ametangaza mageuzi makubwa ya sera punde atakapochukua nafasi ya Barack Obama katika Ikulu ya White House mwezi Januari mwaka ujao.
Bwana Trump, aliyesisitiza vikali kuwa atafutilia mbali bima hiyo inayowapa fursa mamilioni ya Wamarekani maskini kupata huduma ya afya kwa bei nafuu punde tu atakapochaguliwa rais, yaonekana amebadilisha msimamo wake juu ya suala hilo.
Na Katika kile kinachoonekana kulegeza msimamo wake juu ya mpinzani wake Hillary Clinton, Rais huyo mteule amesema,Clinton ni mwanamke mkakamavu na mwenye tajiriba kubwa