Maelfu ya Wananchi wa Cuba wameanza kukubali matokeo kwamba rais wa zamani wa taifa hilo na mwanamapinduzi Fidel Castro hayupo tena na hivyo kuanza kutoa heshma zao za mwisho katika mji mkuu wa nchi hiyo Havana katika mahali palipoandaliwa .

Mwanzo wa maombolezo ya kitaifa kulitanguliwa na mizinga ishirini na moja ishara iliyofanywa pia katika miji ya Havana na Santiago de Cuba, mahali ambako kiongozi huyo alitangaza mapinduzi mnamo mwaka 1959.
Waombolezaji pia walikuwa wakiweka saini za kiapo kuahidi kutekeleza uzalendo na pia kutii kanuni ya ujamaa.kuanzia Jumatano, majivu kutoka katika mwili wake utakao teketezwa yatatembezwa katika nchi hiyo kwa kupita katika vituo vyo alikofanya safari ya mapinduzi ambayo yalimuweka madarakani Fidel Castro .
Na inatarajiwa kuwa siku ya Jumapili majivu ya aliyekuwa Fidel Castro, yatazikwa katika mji wa Santiago.